Amisom waliwaua 6 harusini Somalia
Shirika la kupigania haki za binadamu lenye makao yake makuu huko Washington Marekani,Human Rights Watch (HRW), limesema kuwa majeshi ya mataifa ya muungano wa Afrika Amison yaliwashambulia wageni katika harusi moja iliyokuwa imeandaliwa huko Merka Somalia mwezi uliopita.
Katika ripoti yake mpya shirika hilo la kupigania haki za kibinadamu mpya Human Rights Watch,linasema kuwa wanajeshi wa Uganda walivamia kijiji kimoja ambako kulikuwa na halaiki ya watu harusini.
Waliingia chumbani na kuwatenganisha wanaume na wanawake.'Katika chumba kimoja kilichokuwa na wageni, wanaume 6 walitenganishwa na wanawake na kisha wakawapiga risasi na kuwaua papo hapo.'
'Kati ya wanaume hao sita, wanaume wanne walikuwa ni ndugu baba yao mzazi na ami wao.'
'Wanne walikufa papo hapo kisha mmoja wa ndugu hao aliyejificha chini ya kitanda akawachwa hapo akavuja damu hadi akafa.'
'Walioshuhudia wanasema kuwa wanajeshi hao walikataa kata kata jamaa zao wasiwapeleke hospitalini'' Ripoti hiyo inaeleza.
Kulingana na HRW tukio hilo lilitokea tarehe 31 Julai.
Umoja wa Afrika haujajibu shtuma hizo za HRW.
Shirika hilo la HRW linapendekeza uchunguzi wa kina ufanyike.
'Kuwaua watu bila makosa ili kulipiza kisasi cha mashambulizi dhidi yenu sio jambo jema na hilo litahakikisha kuwa hali itakuwa mbaya zaidi katika siku za usoni ripoti hiyo inasema.
HRW lingali linachunguza ripoti kuhusu mauaji ya raia huko Marka mapema mwezi huu.
Maoni
Chapisha Maoni