Pongezi kwa Issa Machaibya RC Kigoma, kwa kutoa msahada wa chakula na vifaa vya ujenzi katika shule
Ili jamii hapa nchini iweze
kuwa na moyo wa kujitolea katika shuguli za maendeleo inatakiwa kuwepo na
ushirikishwaji wa dhati kati ya viongozi na wananchi ikiwemo motisha hasa pale
inapothibitika baadhi yao wameitikia wito na kushiriki katika kazi za
maendeleo ndani ya jamii.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa
Machibya, ametoa vifaa vya ujenzi na chakula kwa ajili ya shule sekondari
Mugombe iliyoko katika Kata ya Kagezi wilani kibondo, ikiwa ni motisha baada ya
kukuta wamepiga hatua katika ujenzi wa Maabara
Akikabidhi vitu hivyo jana,
kwa niaba ya mkuu huyo wa mkoa katibu tawala wa wilaya kibondo Ayubu Sebabili,
kwa Afisa elimu shule za sekondari Bi Honorata Kabundugulu, amesema kuwa hiyo
ni ahadi aliyoitoa wakati alipokwenda katika ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa
maabara na kukuta wamepiga hatua kubwa shuleni hapo.
Aidha amesema kuwa
zawadi hiyo ni vizuri ukatumika kwa
malengo yaliyokusudiwa na kueleza kwa ni kwa ajili ya kuwahamasisha wananchi
kushiriki katika shuguli za maendeleo na kutaja vitu hivyo kuwa ni pamoja na
Mifuko 30 ya saruji, Sukari kilo mia 1 na mifuko 25 ya unga wa sembe kwa ajili
ya wanafunzi kupata chakula shuleni, vyenye thamani Tsh million 2
Nae Bi Honorata Kabundugulu alipokuwa
akipokea zawadi hizo, amepongeza uamuzi wa mkuu wa mkoa kwani utaongeza ushawishi wa
kushiriki kwa wananchi na watumishi wengine kwenye shuguli za maendeleo huku
mkuu wa shule hiyo Tanu Selemani akishukuru kwa kuwa ahadi hiyo iliahidiwa na
kutekelezwa na kudai kuwa si kwamba wao ni wazuri sana kuliko wengine katika
utendaji
Kwa upande wao wanafunzi wa
shule ya sekondari ya kumwambu wasema kuwa mkuu huyo wa mkoa amefanya vema
kuonyesha mfano wa kuchangia chakula katika
shuleni ya wenzao, kwani swala hilo
limekuwa ni gumu kwa wazazi wengi, hatua inayosababisha wanafunzi kushiriki
masomo kwa shida mara wanapohisi njaa
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni