Wakazi wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wameitaka serikali ijayo kuhakikisha inatatua kero zinazowakabili wananchi katika maeneo mengi hapa nchini hususa kwa wale wanaoishi vijijini ambao kufikiwa na huduma mbalimbali za kijamii ni kwa kususua
Aisha Meda mkazi wa kiyobelas |
Juma Maganga mgombea udiwani kakonko |
Caros Gwamagobe aliyekuwa mgombea ubunge kura za maoni ccm Buyungu |
Christopha Chiiza mgombea ubunge Buyungu akipokea Ilani ya chama cha mapinduzi |
Julias Mbwiga katibu Ccm Kakonko |
Mwinyi Ramadhani mkazi wa kakonko |
Wakazi wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wameitaka serikali
ijayo kuhakikisha inatatua kero zinazowakabili wananchi katika maeneo mengi
hapa nchini hususa kwa wale wanaoishi vijijini ambao kufikiwa na huduma mbalimbali za kijamii ni
kwa kususua
Wakiongea na clouds Tv wananchi hao ambao ni Ramadhan
Mwinyi, Aisha Medas na Juliana Emily, wamesema kuwa hivi wananchi wanakumbwa na
matatizo mengi ikiwa ni kukosa huduma za Afya, Maji, Barabara na Elimu na hata
kutotendewa haki na baadhi ya viongozi wa ngazi za vijiji na kata hatua
inayokwamisha juhudi za maendeleo
Wameeleza kuwa hivi sasa nchi inaelekea kipindi cha uchaguzi
mkuu wagombea wengi wa wanafasi za Urais, Ubunge na Udiwani, wanapita na kutoa
ahadi nyingi kwa wananchi hivyo ahadi hizo kwa wale watakaopata lidhaa hawana budi kuzitimiza kwani kinyume chake ni
kuwakatisha tamaa wananchi
Hata hivyo katika kuzindua wa kampen za uchaguzi ccm Jimbo la Buyungu
wilayani humo, katika harakati za kuwanadi wagombea wake, Katibu wa chama hicho Julias Mbwiga amesema
kuwa ziko changamo hasa katika kukamilisha miundo mbinu ya maji lakini
wamejipanga kuzimaliza kipindi kinachofuata sasa
Kwa upande wake Waziri wa Uwekezaji na uwezeshaji ambaye pia
ni mgombea ubunge jimbo hilo
la Buyungu, amesema kuwa yeye atatumia ilani ya chama hicho japo lipo tatizo la
matumizi mabaya ya fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya huduma
mbalimbali kupitia katika halmashauri ya wilaya akaahidi kusimamia ili
mafanikio yawepo
Jimbo hilo
kupitia vyama mbalimbali lina wagombea wa nafasi za ubunge watatu ikiwa ni
Metusela Atanas NCCR Mageuzi, Samson Bilago CHADEMA na Christopha Chiiza
kupitia CCM
Maoni
Chapisha Maoni