Shule ya msingi Nengo ya Walemavu, iliyoko wilayani Kibondo mkoani kigoma, inayohudumia wanafunzi walemavu wa mahitaji maalum inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni ukosefu wa maji Vifaa vya kujinfunza na kufundishia na vyombo vya kulia chakula
Wanafunzi shule ya msingi Nengo elimu maalum walemavu |
Elisha George mwanafunzi shule ya msingi nengo walemavu |
Lukas Frand muu wa shule ya Nengo |
Islafil Ntoteye mwenyekiti chama cha walemavu wa ngozi w kibondo |
Shule ya msingi Nengo iliyoko
wilayani Kibondo mkoani kigoma, inayohudumia wanafunzi walemavu wa mahitaji
maalum inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni ukosefu wa maji Vifaa vya kujinfunza na kufundishia na vyombo
vya kulia chakula
Akisoma lisara kwa niaba ya
wanafunzi wenzake wakati wa afla ya matembezi kwa ajili ya kutoa elimu juu ya
kuwatambua na kuwa thamini walemavu yaliyoandaliwa chama cha walemavu wa ngozi
Tas kwa kuzishirikisha baadhi ya shule
za sekondari za mjini kibondo Elisha
George ambaye ni mlemavu wa macho, hali inayoweza kusababisha kiwango cha elimu
kushuka
Ameeleza kuwa kwa wanafunzi ambao si walemavu wa viungo
wanatumia muda mrefu kuchota maji badala ya kusoma, kwa ajili ya kuwasaidia
wenzao wasiyokuwa na uwezo kulingana na
viwango vya ulemavu walivyonavyo
Hata
hivyo wameongeza kuwa wakati wa kupata chakula hawezi kupata chakula hicho kwa
pamoja kwasababu ya ukosefu wa vyombo hali ambayo uwalazimu kubiliana huku
wakiiomba serikali kulitazama swala hilo
na kuomba kupatiwa vitabu kwa ajili ya kujifunzia vikimo vya nukta nundu kwa wasioona
Mkuu wa shule hiyo Bw Lukas
Frandy amesema kuwa fedha inayotolewa kuendesha shule hiyo ni kidogo sana
kulingana na hali za watoto wenyewe na
wengine uri wao ni mdogo sana ulio chini ya miaka mitano na kudai tatizo kuwa
ni jamii kubwa hapa nchini, inakosa elimu mahususi ya kuwatambua na kuwathamini
watato walemavu kuwa hata wao wanaweza hali inayoonekana
Pamoja na mambo mengine
mwenyekiti wa chama cha walemavu wa Ngozi Tas wilaya kibondo Bw, Islafil
Ntoteye katika taarifa yake kwa jamii
amesema kuwa kwa upande wa walemavu wa ngozi kuwa hiyo ni hali ya kawaida kwa binadamu kukosa vinasaba ambavyo upelekea kuzaliwa mtu
Albino kuitaka jamii kuachana na tabia kuwaita Dill, Biashara au Zeruzeru, huku
Filbert Misuzi ambaye alimwakilisha mkurugenzi wa Halmashauri akiitaka jamii
kupeleka watoto shule ili waelimike na kuondokana na dhana potovfu za
ushirikina
Akijibu lisara hiyo
mwakilishi wa mkuu wa wilaya kibondo ambae alikuwa mgeni rasmi katika sherhr
hiyo, mkaguzi wa jeshi la Polisi Tanzani
Fotunatus Fransis amesema kuwa matatizo hayo atayafikisha kwenye ofisi husika,
na kulingana hali hiyo ya kuwindwa kwa kundi la walemavu wa ngozi amesema jeshi
hilo linaadaa mpango wa kuwa wanakutana wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari ili kutoa elimu juu ya ulinzi shirikishi
Kasim Fatilo afisa elimu
maalum amesema vifaa vya kufundishia
katika elimu maalum ni bei kubwa hivyo wamefanya utaratibu kuomba wizara ya
elimu, na upande wa maji ameeleza kuwa maji yanapo katika ndo wanafunzi wengine
ulazimika kuchata maji kwa ajili ya matumizi
Shule zilizoshiriki katika
matembezi hayo ni Bishop mpango sekondari, Tutuba , shule ya sekondari ya
wasichana kibondo, na Mount
Chanza sekondari
Maoni
Chapisha Maoni