Viongozi wa Vijiji na Kata simamien na kutoa elimu umuhimu wa Lishe
Kibondo.Viongozi wa Kata na
Vijiji wamehaswakuendelea kuhamasisha umuhimu wa Lishe na mpangilio wa matumizi
ya vyakula kwa Watoto na watu rika zote ukiwemouchangiaji wa chakula Mashuleni
ili kupunguza udumavu na kuinua kiwango cha Elimu
Amebainishahayo Afisa Lishe Wilaya ya Kibondo Tumaini Muna
wakati wa kujadili ripoti ya utekelezaji afua za Lishe kwa robo yanne 2025/26
ambapo ameeleza kuwa licha ya shule zote kutoa huduma ya Chakula,wapo baadhi ya
Wazazi ambao hawachangii chakula kwaajili ya Watoto waojambo ambalo halikubaliki
Aidha Munna ameongeza kuwa ili kukabiliana na changamo ya
udumavu,ni lazima afua za lishe zisimamiwe kikamilifukuanzia ngazi za familia
huku akisistiza viongozi kusimamia kwa Vitendo mafunzo yanayotolewa katika
maadhimisho ya siku ya Afya ya Lishe ya Kijiji
‘’Hatuwezi kufikia malengo pasipo kwenda pamoja hivyo hao wazazi
ambao hawajitolei katika uchangiaji wa huduma ya chakula wanakwenda kinyume
hivyo elimu na usimamizi ni muhimu kwani wanaopata shida ni Watoto maana Mtoto
kushinda njaa kuanzia asubuhi hadi alasiri ni kumdhoofisha’’ amesema Muna
Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo
Kanal Aggrey Magwaza amesema uthabiti wa upatikanaji wa chakula mashuleni
utasaidia kupunguza mdondoko kwa Wanafunzi na upatikanaji wa chakula utaongeza
hamasa kwa Wanafunzi kupenda kuudhuria masomo
Nao wajumbe wa Kikao hicho wameahidi kuendelea kushirikiana kwa
pamoja kuhamasisha upatikanaji wa chakula mashuleni




Maoni
Chapisha Maoni