Wizara ya Viwanda kushirikiana na Taasisi zingine zenye nia ya kuanzisha Biashara

 



















Wizara ya Viwanda na Biashara imesema itaendelea kushirikiana na taasisi nyingine za serikali kuweka mazingira rafiki kwa wale wote wenye nia ya kuanzisha biashara katika mkoa wa Kigoma, wanafanikiwa kufanya hivyo kwa kuwapatia motisha na upendeleo maalum ambao upo kisheria.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Dennis Londo, wakati akifungua Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara (Lake Tanganyika International Expo 2026), yanafanyika katika viwanja vya Mwanga Community Center mkoani Kigoma kwa kauli mbiu isemayo ‘Kigoma ni Kisima cha Fursa na Uwekezaji’.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua, ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwenye ufunguzi wa maonyesho hayo, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji.

Balozi wa Ubalozi Mdogo wa Burundi mkoani Kigoma, Kekenwa Jeremiah, amesema maonyesho ya biashara ni zaidi ya mahali pa kufanyia miamala ya fedha bali mahali ambapo tamaduni hukutana na mawazo huungana ili kuchochea maendeleo, huku Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Ndg. Hassan Rugwa akiwataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo Kigoma.

.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI SGR NA KUZINDUA MELI NNE ZA MIZIGO ZIWA TANGANYIKA

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu