VIJANA ONGEZENI MAARIFA

![]() |
| Roberth Kihwele Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibondo |
![]() |
| Abeli Mbilinyi Mwakilishi Shirika la Enabel katika Mahafali FDC Kibondo |
![]() |
| Polo Ayoub Afisa Tarafa Kibondo, Mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kibondo kwenye Mahafali Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibondo |
Vijana waliokosa Elimu na
wale waliokuwa nje ya mfumo wa Elimu kisha kupatiwa fursa na Serikali na kuanza
kupata mafunzo ya ufundi ya muda mfupi katika vyo mbali mbali hapa nchini
wameshauriwa kujiendeleza pale watakapokuwa wamepata nafasi hiyo ili kuongeza
maarifa zaidi
Ushauri huo umetolewa na
Afisa Tarafa ya Kibondo
MkoaniKigoma,Polo Ayubu kwa niamba ya Mkuu wa Wilaya ya Kibondo wakati wa kufunga mafunzo ya miezi sita katika
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibondo na kuwataka kuwa na uhitaji wa kuongeza
maarifa zaidi
Amesema kuwa ulimwengu unabadili na mambo yanakuwa
tofauti hivyo ili kwenda na kasi sitaiki hawatakiwi kuridhika na hatua hiyo ya
mafunzo bali wajiendeleze ndipo watapofurahia zaidi fursa ya mafunzo hayo
Vijana waliopata nafasi
katika chuo hicho, wamepata mafunzo hayo kupitia Mradi wa wezesha Binti
unaofadhiliwa na Shirika la Enabel ambapo mwakilishi wa Shirika hilo Abel
Mbilinyi amesema hatua hiyo itasaidia
vijana wengi kujiajili
Aidha Mbilinyi amesema kwa
kutambua hilo Enabelinashirikiana na Vyuo saba katika Mkoa wa kigoma
kuwawezesha Vijana kupata maarifa ili waweze kujikimu katika maisha yao ya
baadae
Hata hivyo Mkuu wa Chuo
cha Maendeleo ya Wananchi Kibondo Robath Kihwele amesema fursa hiyo. Imesaidia
kuongeza maarifa hata makundi yaliyofikiriwa kuwa hayawezi kama Wasichana
katika kupata ujuzi tofauti
Nao baadhi ya Wahitimu
katika lisara yao wamesema mafunzohayoyatakuwa chachu katika maisha yao kwani
wengi wamekuwa wakikosa fursa mbalimbali kutokana na uwezo mdogo wa kiuchumi
lakini wao kwa sasa wataweza kujiajiri na hata kuajiriwa pia, huku wakitoa
shukrani zao kwa shirika la Enabel na Serikali ya Tanzania
Kihwele ameongeza kuwa
kumekuwepo mawazo hasi kutoka kwa baadhi ya Wazazi na walezi wakiwa vikwazo
Watoto wao kutowaruhusu kusoma taaluma kama za umeme na Magari kwa wasichana
ikifikiriwa kuwa fani hizo zinawavunjia heshima Wasichana, wakati ni fani kama
zingine ili mradi Kijana ajitambue yeye mwenyewe





Maoni
Chapisha Maoni