Mahakamani kwa kujifanya Afisa wa usalama wa Taifa
Mahakamani kwa kujifanya Afisa wa usalama wa Taifa Mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es salaam amehukumiwa kifungo cha miezi 24 jela au faini ya shilingi laki moja na nusu katika mahakama ya wilaya ya kibondo mkoa wa kigoma, baada ya kukili makaosa ya kujifanya mtumishi wa serikali wa jeshi la wananchi Tanzania na kujifanya afisa usalama wa taifa Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya kibondo bw Erick Marley mwendesha mashitaka wa polisi bw Frank Ruvanda amemtaja mtu huyo kuwa ni Wiston Ezekiel Bulinjie mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa kinyerezi dar es salaam Bw Ruvanda amesema kuwa mnamo Agost 12 mwaka huu majira ya saa 9 alasiri bw Bulinjie alikwenda kikosi cha 824 KJ kanembwa Jkt wilayani kakonko alijitambulisha kwa Erast Sebasitian Tesha kuwa yeye ni askari wa jeshi la wananchi Tanzania kitu ambacho hakikuwa cha kweli , tarehe hiyo hiyo majira ya saa11 jioni akiwa kibondo mjini alijitambulisha kwa Godifrey Mpigwa kuwa yeye ni afisa usalama wa taifa K...