Serikali yatakiwa kuandaa utaratibu wa ajira kwa wanaomaliza JKT

Majar Castory Bwegoge mkuu wa Kikosi 824 kj Kanembwa jkt
Baadhi ya wahitim JKT
Wahitimu JKT wakiwa kwenyeGwaride



Mwemezi Muhingo  Kanembwa Kakonko

Serikali imeshauriwa kuweka utaratibu wa ajira kwa Vijana wanaohitimu mafunzo ya Kijeshi katika Jeshi la kujenga Taifa JKT mara baada ya mikataba yao ya miaka miwili kuisha

Hayo yamesemwa na  wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi Vijana wa kujitolea na wa Mujibu wa sheria, Oparation miaka 50 ya Muungano,  katika jeshi la kujenga Taifa, Kikosi cha 824 KJ Kanembwa JKT  kilichoko Wilaya ya kakonko Mkoa wa Kigoma, yalipokuwa yakifungwa rasmi

Katika Lisara yao iliyomwa na Dora Damasi ambae ni mhitimu jkt, wamesema kuwa ni vizuri serikali kupitia jeshi hilo, kuandaa utaratibu kwa vijana wanaomaliza mafunzo yao mara baada ya mikataba kuisha ndani ya jeshi la kujenga Taifa  ili wapatiwe ajira katika Taasisi za  serikali hapa nchini kama Jeshi la ulinzi Tanzania, Takukuru Polisi na nyinginezo ili kuondoa usumbufu  wanaporudi majumbani kwao.

Insert 1 Dora Damasi msoma lisara mhitimu JKT
Que in……………………

Aidha wamesema ili kuweza kudumisha muungano nizuri vijana wa mujibu wa sheria yaanai wale wanaokuwa wamemaliza kidato cha sita kutoka Zanzibar wapatiwe fulsa za kujiunga na jeshi la kujenga Taifa katika vikosi vya Tanzania Bara na wanzao wa Bara, wajiunge na Jeshi la kujenga Uchumi la Zanzibar JKU.ili kuleta usawa.


Nae mkuu wa kikosi hicho cha Kanembwa JKT, Major Castory Bwegoge amesema kuwa vijana hawa waliohitimu mafunzo ya kijeshi wamepatiwa mafunzo mbalimbali kwa nadhalia na kwa vitendo kwa mujibu wa sirabi yao na kufaulu katika viwango vinavyokubalika, hivyo wale wote wa kujitolea watapelekwa katika vikosi mbalimbali na makambi hapa nchini ili kuendelea kujifunza staid za kazi na ujasriamali ili wawe na uwezo wa kujiari baada ya mikataba yao kuisha


Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa JKT  Taifa Luten Festusi Mawella ametoa wito kwa vijana hao waliohitimu mafunzo ya kijeshi kuzingatia kiapo walichikitoa mbele ya mgeni rasm na Amili jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini na kujua kuwa mafunzo waliyoyapa ni kwa manufaa ya watanzania wote na siyo kwa manufaa binafsi maana hakuna mtu yeyote kutoka nje atakayetusaidia kuijenga nchi hii.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa kigoma Kanal Mstaafu Issa Machibya, ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga manzo hayo,  amesema kuwa lengo la kuanzisha jeshi la kujenga Taifa ni kuwa na mtanzania aliyepevuka kwa ajili ya kuleta mshikamo na maendeleo ya Taifa na kumudu maisha   maisha katika Amani na utulivu

Aidha Machibya amesema kuwa niwajibu wan chi kuwapitsha vijana wake katika Jeshi la kujenga Taifa  ili kuwaanda kuwa viongozi bora na wazalendo wa kweli wan chi yao na kuwafunza kuwa namoyo wa kujiamini kuwa wanaweza kujitegemea katika maisha yao na kuwataka wakumbuke yote waliyojifunza kwa kuyatendea kazi



  Nao wahitimu wa mafunzo hayo wameeleza waliyojifunza kuwa ni mengi hasa upande wa ujasriamali na kudai kuwa ujasriamali ni kujiari mwenyewe bila kutegemea upande wowote  na jinsi watakavyofanya baada ya kuelekea watakakopangiwa na wengine kuendelea na masomo yao katika vyuo mbalimbali hapa nchini



Katika mwaka huu 2014 wamehitimu jumla ya vijana 2166 ikiwa wa kujitolea ni wale wakujitolea na mujibu wa sheria ambapo wavulana ni 1685 na Wasichana  481 katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa Jkt
Mwisho


Issa Machiby mkuu wa mkoa wa kigoma aliyekuwa mgeni rasmi katika ungaji wa mafunzo ya kijeshi Kanembwa JKT

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao