Mahakamani kwa kusababisha kifo kwa kumpa muwa unaosadikiwa kuwa na sumu
Mahakamani kwa kusababisha
kifo kwa kumpa muwa unaosadikiwa kuwa na sumu
Mkazi wa kijiji cha kumsenga wilayani kibondo mkoani kigoma
amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya kibondo kwa tuhuma za mauaji ambapo
inasadikika kuwa alimpa muwa wenye sumu bw Matane Ndegea na kusababisha kifo
chake
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya kibondo bw
Mulokozi Kamuntu mwendesha mashitaka wa polisi bw Frank Ruvanda amemtaja mtu
huyo kuwa ni Sintegeza Ally mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa kijiji cha kumsenga
Bw Ruvanda amesema kuwa mnamo September 08 mwaka huu majira
ya saa tisa alasiri bw Sintegeza ally
kwa makusudi alimuua bw Matane
Ndegea kwa kumpa muwa wenye sumu ambao ulipelekea kifo chake
Hakimu mkazi bw Kamuntu ameahilisha kesi hiyo mpaka itakapotajwa
tena September 30 mwaka huu na mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa
mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauji hivyo mshitakiwa yuko
rumande kutokana na kwamba kesi yake haina mdhamana
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni