Wazazi wakataa kuchangia chakula shuleni
Mwemezi Muhingo Kakonko
Baadhi ya wananchi wa kata ya Nyamtukuza wilaya ya kakonko
mkoani kigoma wamaepokea kwa mawazo tofauti swala la uchangiaji wa chakula cha
wanafunzi mashulenim, baada ya mkuu wa
wilaya hiyo Bw, Peter Toyima kuagiza kwenye mkutano wa hadahara kuwa nilazima
watoto wote wapate chakula mashuleni.
Wakazi wa kata hiyo wameiambia clouds Tv kuwa wengi wao hawana uwezo wa kiuchumi na
wanakabiliwa na tatizo la hali ya hewa
wakati wa msimu wa kilimo hali inayowafanya wapate mavuno kidogo na kushindwa
kuendesha vizuri familia zao
Wamedai kuwa hawawezi kuchangia chakula hicho bali ni vizuri
utarati wa zamani uendelee huo huo, wa watoto kula majumbani mwao baada ya
masomo
Aidha wamesema kuwa nikweli mpango huo ni mzururi ila
ungefanyika utaratibu wa utoaji wa chakula kwa awamu ili kuepuka kuwaumiza
baadhi ya wazazi na familia zao kwakuwa wengine kipato chao ni kidogo
Mkuu huyo wa wilaya ya kakonko amesema kuwa kuna mambo mengi
yanayochangia kushuka kwa kiwango cha elimu katika shule za msingi na sekondari
ikiwemo wanafunzi kutokupata chakula cha mchana mashuleni hali inayowafanya
watoto kutokufatilia masomo ipasavyo
Maoni
Chapisha Maoni