Mahakamani kwa kujifanya Afisa wa usalama wa Taifa
Mahakamani kwa
kujifanya Afisa wa usalama wa Taifa
Mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es salaam amehukumiwa kifungo
cha miezi 24 jela au faini ya shilingi laki moja na nusu katika mahakama ya
wilaya ya kibondo mkoa wa kigoma, baada ya kukili makaosa ya kujifanya mtumishi
wa serikali wa jeshi la wananchi Tanzania na kujifanya afisa usalama wa taifa
Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya kibondo bw
Erick Marley mwendesha mashitaka wa polisi bw Frank Ruvanda amemtaja mtu huyo
kuwa ni Wiston Ezekiel Bulinjie mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa kinyerezi dar
es salaam
Bw Ruvanda amesema kuwa mnamo Agost 12 mwaka huu majira ya
saa 9 alasiri bw Bulinjie alikwenda kikosi cha 824 KJ kanembwa Jkt wilayani
kakonko alijitambulisha kwa Erast Sebasitian Tesha kuwa yeye ni askari wa jeshi
la wananchi Tanzania kitu ambacho hakikuwa cha kweli , tarehe hiyo hiyo majira
ya saa11 jioni akiwa kibondo mjini alijitambulisha kwa Godifrey Mpigwa kuwa
yeye ni afisa usalama wa taifa
Kesi hiyo ilikuwa inakuja kwa ajiri ya kutajwa ndipo
mshitakiwa akaomba akumbushwe makosa yake na baada ya kukumbushwa alikili
kutenda makosa hayo kisha hakimu mfawidhi Erick Marley akamuhukumu kifungo cha
miezi 24 au kulipa faini ya shilingi laki moja na nusu kwa makosa yote mawili hata
hivyo mtuhumiwa amelipa faini hiyo na
kuachiliwa huru
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni