Mahakamani kwa kuendesha gari kizembe na kusababisha vifo

Mkazi wa mwanza aliyekuwa anaendesha basi lililopinduka na kuuwa watu wawili wilayani kakonko mwanzoni mwa wiki iliyopita amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya kibondo na kufunguliwa kesi ya usalama bara barani namba 19 ya mwaka 2014 kisha kushitakiwa kwa makosa saba likiwemo la kusababisha vifo kwa uendeshaji wa gari  kizembe

Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya kibondo bw Esmael Ngaile mwendesha mashitaka wa polisi bw Frank Ruvanda amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa nib w Kalim Suleiman kwa jina maarufu msangi  mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa jijini mwanza

Bw Ruvanda amesema kuwa mnamo Septemba 08 mwaka huu majira ya saa tano na nusu asubuhi katika bara bara ya kakonko nyakanazi eneo la kanyonza mtuhumiwa alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajiri T 273 ACX aina ya Scania bus kutoka kigoma kwenda kahama  na aliendesha gari hilo kwenye bara bara ya umma kwa uzembe na kushindwa kulimudu na hatimae kupinduka

Aidha bw Ruvanda amesema kuwa mtuhumiwa ameshitakiwa kwa makosa saba ambapo mawili ni ya kusababisha vifo , kosa moja la kusababisha uhalibifu wa gari kwa uendeshaji wa kizembe pamoja na makosa manne ya kusababisha majeruhi kwa abilia kutokana na uendeshaji gari kizembe

Amesema kuwa abiria waliofariki katika ajali hiyo ni marietha Obed na mwanae Mudi Rashidi ambao tayari miili yao imesafirishwa kwenda kigoma na waliojeruhiwa kwa kiasi kikubwa ni masanja wandule , pendo john , Maua Noni , pamoja na Minza Kilungura ambao wote tayari wameendelea na safari zao  baada ya kutibiwa majeraha yao

Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya kibondo bw Ismael Ngaile ameahilisha kesi hiyo mpaka itakapo tajwa tena octoba 03 mwaka huu ikiwa ni kupisha upelelezi Zaidi  wa tukio hilo na mshitakiwa yuko nje kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya dhamana
Mwisho 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao