Ni jambo lililozoeleka kwa sabuni zenye dawa kuuzwa mitaani, badala ya kwenye maduka maalumu. Uuzwaji huu wa kiholela usiozingatia afya ya mtumiaji unaweza kuwa na athari bila muhusika kufahamu. Gazeti hili limebaini kuwa wengi wa wanaonunua sabuni hizo, kama Dettol, Rungu, Family na Life Bouy, hawanunui kwa ajili ya tiba badala yake hununua kulingana na zinavyonukia na zinavyotoa taka mwilini. Endrew Mlungu, mkazi wa Buguruni Dar es Salaam, aliyekuwa akinunua sabuni hizo maeneo ya Buguruni Chama, alisema kuwa anapenda kutumia Life Bouy kwa sababu akiogea zinamtakatisha na huziona taka zikimtoka wakati anajisugua. Anasema pale hali yake ya kifedha inapokuwa si nzuri, hutumia sabuni nyingine lakini akiwa nazo anainunua kwa kuwa humuacha mwepesi na akioga, hufanya kweli. “Nikiogea sabuni tofauti na hii najisikia kama sijaoga na hata nikiangalia sakafuni wakati najisugua sioni taka kwa maana hiyo hazitoi na hazinisafishi vizuri,” anasema Mlungu. Mlungu anafafanu...
Maoni
Chapisha Maoni