halmashauri yatakiwa kusitisha zuio la uuzaji wa mkaa kabla ya kupatikana nishati mbadala
Rojas Kosmas meneja misitu kibondo |
nicolaus kirunga katibu chadema wilaya ya kibondo |
Chama cha Demokrasia na
Maendelo CHEDEMA, wilaya Kibondo mkoani
Kigoma kimeitaka Halmashauri ya wilaya hiyo kupitia Idara ya Misitu, kuondoa
katazo la uuzaji wa mkaa na kuni kwa wachuuzi wadogowado kabla ya kupatikana
kwa nishati mbadara ili kuepuka usumbufu katika jamii.
Akiongea na Waandishi wa habari
Mwenyekiti wa Chadema wilayani humo. Nichaus Kilunga, amema wakazi wengi wa
kibondo mjini na vijijini, wanatumia nishati ya mkaa na kuni hivyo kuwazuia
gafra bila kuwa na maandalizi ya kielimu
na tahimini za kiuchumi kwa jamii husika
ni kuleta adha kwa wanannchi wanaotegemea mahitaji hayo kwa matumizi yao ya kila siku
Asemema kuwa ni vizuri kabla ya
kutumia nguvu Idara ya misitu itoe elimu
kwa wahusika, na kuhakikisha nishati mbadara inanapatikana ndipo utekelezaji
ufanyike kuliko kufanya jambo kwa haraka ambalo litawagusa wengi na kusababisha
malumbano yasiyokuwa na ulazima.
Aidha amesema sasa uongozi wa
Halmashauri kupitia Idara ya misiti wilayani humo iondoe zuio hilo, kasha ikae na wauzaji na watumiaji wa mazao hayo ya
misitu ili elimu itolewe juu ya utunzaji wa mazingira na tozo zote za mazao ya
misitu na watu wote waweze kelewa ni jlipi la kufanya
Kwa upande wake Katibu wa Chama
hicho wilayani humo, amedai kuwa kwa kuendeleza zuio hilo, bila utaratibu
maalumu ni kukiuka haki za Binadamu kwa kuwa hali hiyo inawanyima watu mahitaji
yao ya lazima
Nao wafanyabiashara ya mkaa
wamesema kuwa hatua hiyo iliyotangazwa tarehe 13/ agust 2014 kuwa ifikapo agust 18 /2014 hakuna mtu yeyote
atakayeruhusiwa kutembeza mkaa mitaani kwa ajili ya biashara bali kila mtu
akatafute kibali, imewafanya waishi kwa kuhangaika kwa sababu tangazo hilo
limetoa muda mfupi sana kwakuwa garama
za kupata vibali hivyo shilingi laki 2 na 60 ni kubwa kulingana na kipato chao
Watumiaji wa bidhaa hiyo ambayo
inaonekana kuwa adimu kabisa siku hizi, na kuuzwa kwa bei kubwa ya shilingi 50,000 kila gunia, tena usiku wa manane wanaeleza adha ambazo
wanakumbana nazo kwa sasa kutokana na watu ambao wamekuwa wakiiuza kwa
kutembeza katika mitaa mbalimbali mjini kibondo.
Kwa upande wake meneja
Misitu wa wilaya hiyo Rojas simony
alipoulzwa kuhusu swala hilo amesema kuwa nikweli jambo hilo lipo ila watu
walitaarifiwa mapema juu ya utaratibu unaotakiwa kwa wafanyabiashara wa mazao
ya misitu kulingana na sheria na
nataratibu
Hata hivyo amedai kuwa wauza mkaa na watumiaji watahathirika ila
yeye hawezi kuacha sheria inavunjwa huku akiwa anaona, pamoja hali kuwa ngumu
kwa walengwa na hakuna aliyezuiliwa kufanyabiashara bali kinachotakiwa ni
kufuata sheria zilizowekwa
Nishati hiyo ya mkaa na kuni
imeonekana imeanza kuuzwa kwa magendo mjini humo, tena kwa bei kubwa hali
ambayo imelalalamikiwa na baadhi ya wuzaji na watumiaji, kabla ya zuio, gunia
moja la mkaa lilikuwa linauzwa shilingi 15000/ ila hivi sasa linauzwa kiasi cha
shilingi 50,000/ garama ambayo imeonekana kuwa kubwa zaidi
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni