Mwanafunzi wa Darasa la tatu abakwa,
Mwanafunzi wa Darasa la tatu abakwa,
Mwanafunzi wa Darasa la tatu katika shule ya Msingi
Busunzu B Wilayani Kibondo amelazwa katika hospitali ya Wilaya hiyo
baada ya kubakwa na kijana mmoja
alietajwa kwa jina la Lukelegwa Maneno Mkazi wa Kijiji cha Busunzu B.
Akizungumza na na waandishi wa habari , Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya
ya Kibondo Mkoani Kigoma Dr. Adam Jonathani amesema mtoto huyo wa Kike mwenye umri wa Miaka
10, amepata majeraha makubwa na
inaonyesha amechomwa na kitu chenye ncha kali sehemu zake za sili baada ya
kubakwa.
Dr. Jonathani amesema mtoto huyo hali yake
inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu hospitalini hapo na kwamba kwa
sasa wanaendelea kumtibu Ugonjwa wa
Maralia uliongundulika katika hatua za uchunguzi wa awali.
Hata hivyo Dactari huyo hakuwa tayari kuzungumza kwa uwazi juu ya hali halisi ilivyo kulingana
na uchunguzi ulifanywa na waganga wa hospitali hiyo juu ya huyo mtoto.
Aidha jeshi
la polisi Wilayani Kibondo limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba
juhudi za kumfikisha mahakamani mtuhumiwa aliyehusika katika tukio hilo
zinaendelea baada ya kukamilisha ushahidi.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni