Aua Mwanafunzi ala Ubongo, Aijikata sehemu za siri

Aua mwanafunzi, ala ubongo, ajikata uumeFRANCIS Fortunatus (9), mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Marangu Hills Academy, ameuawa kinyama na mtu anayedaiwa kuwa mfanyakazi wao baada ya kumcharanga kwa mapanga kichwani na kisha kula ubongo wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Robert Boaz, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Alisema mwanafunzi huyo alifariki dunia juzi majira ya saa 1:20 asubuhi nje ya lango la kuingilia nyumbani kwao, Kijiji cha Samanga, Kata ya Marangu Mashariki.

Kamanda Boaz, alisema muuaji ametambuliwa kuwa ni Lawrence Mramba (22), ambaye inadaiwa alishikwa na mapepo yaliyosababisha pia kukata uume wake na kuanza kuutafuna kabla ya kupoteza maisha baada ya kufikishwa Hospitali ya Kilema, Moshi Vijijini.

“Polisi tunaendelea na uchunguzi wa kina wa kifo hicho, lakini mtuhumiwa wa mauaji hayo, baada ya kumuua mwanafunzi huyo aliamua pia kujikata kwa panga sehemu zake za siri. Miili ya marehemu hao imehifadhiwa Hospitali ya Kilema,” alisema Kamanda Boaz.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Venessy Mallya na Obed Shayo, wakati mauaji hayo yakitokea, baba mzazi wa mtoto huyo, Fortunatus Urassa, alikuwa safarini eneo la Marangu-Mtoni akienda mkoani Singida anakofanyia shughuli zake za kibiashara.

Tanzania Daima ilimtafuta kwa njia ya simu mzazi huyo, ambaye alisema kuwa Lawrence alikuwa mwanafunzi wake wa kozi ya useremala, ambaye pia alikuwa akimtumia kama fundi wake msaidizi.
“Huyu kijana alikuwa mfanyakazi wangu na wakati alipomaliza mafunzo yake, niliamua kumuajiri kama fundi… inashangaza kwa sababu sikuwahi kujua kama alikuwa mgonjwa wa akili wala kubaini ukorofi wake kazini,” alisema mzazi huyo kwa masikitiko.

Mkuu wa Shule ya Marangu Hills Academy, Thomas Malulu, alisema kuwa mwanafunzi huyo aliuawa akiwa njiani kwenda shuleni hapo, takribani mita 100 kutoka lilipo lango kuu la kuingilia shuleni.
Alisema baada ya kumtambua marehemu kuwa ni Francis Fortunatus, walimsaka muuaji huyo na kumkuta akiwa amejificha karibu na nyumbani kwa marehemu akiwa ametapakaa damu baada ya kujifyeka uume wake.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji