SWALA kuanza utafiti upatikanaji nishati
KAMPUNI ya Mafuta na Gesi ya Swala (Tanzania), imetangaza rasmi kuanza kwa mpango wake wa mwaka 2014 kuanza utafiti wa upatikanaji wa nishati ujulikanao kama 2D.
Lengo la utafiti huo ni kusaidia kupata taarifa za nishati zitokanazo na tetemeko la ardhi kwenye bonde la Moshi, mpango ambao upo ndani ya leseni ya utafutaji nishati Pangani Kaskazini mwa Tanzania.
Akizungumzia kuanza kwa utafiti huo mwanzoni mwa wiki hii, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, David Rigde, alisema utafiti huo wa nishati itokanayo na matetemeko ya ardhi, unafanywa kama mwendelezo wa mpango uliyowahi kufanikiwa kwa kiasi kikubwa ndani ya maeneo hayo yenye leseni mwaka 2013, ambayo matokeo yalionyesha kwamba angalau bonde moja lina mrundikano wa mchanga wenye unene wa mita 3,000,430.
Aidha, utafiti huo wa nishati itokanayo na matetemeko ya ardhi unafanywa kama mwendelezo wa mpango uliowahi kufanikiwa kwa kiasi kikubwa ndani ya maeneo hayo yenye leseni ya mwaka 2013 ambapo matokeo yalionyesha kwamba angalau bonde moja lina mlundikano wa mchanga wenye unene wa mita 3,000.
Alibainisha kwamba, madhumuni ya utafiti huo mpya ni kuwawezesha wabia kulielewa bonde hilo na kuweka mbinu mkakati ambazo zitawezesha katika shughuli za uchimbaji mwaka 2015.
Maoni
Chapisha Maoni