wananchi wapongeza uongozi wa hifadhi ya taifa Arusha
bi Mary Kilombo mwana ikolojia hifadhi ya taifa arusha |
bw Nathanael shafuni mhifadhi mkuu hifadhi ya taifa arushwa |
Mwemezi Muhingo Arusha
Baadhi ya Wananchi wa kijiji
cha Ngarenanyuki wilayani Arumeru, Mkoa wa
Arusha, wameupongeza uongozi
wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha kwa huduma wanazozipata kutokana na Hifadhi hiyo,
Hayo yamesemwa na wakazi hao
wanaoishi kwa kwenye vijiji ambavyo vinaizunguka hifadhi hiyo, wakati wa ziara
ya waandishi wa habari wa mkoa wa Kigoma walipotembelea na kuona baadhi ya kazi
zinazofanyika humo.
Wakazi hao wamesema kuwa
kushirikiana na huongozi wamekuwa wakipatiwa ajira ndogondo za mara kwa mara
ambazo zinawasaidia kuongeza pato katika familia zao ikiwa ni pamoja na
kuwasindikiza watalii wakati wa kupanda mlima Meru ikiwa ni pamoja na na kujengewa shule katika maeneo ya vijiji
vyao na huduma za Afya zinazopatika hifadhini.
Pamoja na faida wanazozipata
wametaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni wanyama kutoka ndani ya
hifadhi na kushambulia mazao yao
mashambani hali inayorudisha nyuma maendeleo katika shughuli za kilimo.
Hata hivyo mkuu wa Idara ya Ujirani mwema wa Hifadhi ya Taifa
ya Arusha, Bw, Nathanael Shafuni, amesema kuwa Idara yake na Hifadhi kwa ujumla,
inakabiliana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wakzi hao ambao wanaishi
karibu kuwa kutafuta kuni za kupikia na kutaka kitoeo hali ambayo ni kinyume na
taratibu lakini wanajitaidi kutoa elimu.ili waweze kuelewa na kuithamini
hifadhi
Aidha amesema kuwa wamekuwa
wakitoa elimu kwa wananchi hao waweze kuithamini hifadhi na kujua kuwa ni mali yao
na na Taifa kwa ujumla hatua iliyopelekea kuwashirikisha katika shughuli
mbalimbali za kufanya ili kujiongezea kipato cha familia
Kwa upande wake mkuu wa
Hifadhi hiyo Bi, Maria Kilombo wamewataka Watanzania kuendelea kujijengea tabia
ya kufanya utalii wa ndani katika za Hifadhi zilizopo hapa nchini na kuondoa
tabia ya kusema kuwa hiyo ni kazi ya wazungu kwani hata wao ni yao na wanaongeza pato la
Taifa na kutaja idadi ya watalii wandani kufikia mwaka 2012/2013
Maoni
Chapisha Maoni