ILEMELA KUENDELEA KUIMARISHA MTANDAO WA BARABARA
![]() |
| Moja ya eneo la Barabara zinazojengwa na Tarura Kiwango cha Lami Kagua Nyamhongo Mwanza |
![]() |
| Stephan Malimi |
![]() |
| Bahati Ezekiel Mwananchi |
![]() |
| Sobe Makonyo Meneja wa Tarura Wilaya ya Ilemela |
Ujenzi wa Barabara za Busweru
Busenga km 3 na Buswelu Kagua hadi Barabara kuu ya Mwanza Musoma kilomita 9 ni
moja ya hatua ambazo zimesaidia kuondoa changamoto ya mawasiliano ya maeneo
tofauti na kurahisha usafiri kwa
Wananchi Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza
Baadhi ya Wakazi Wakagua, wameeleza kuwa awali wamekuwa wakipata shida
kubwa ya kusafirisha wagonjwa kwenda hospitali wakati mwingine vilitokea vifo
kwa watumiaji wa vyombo vya Moto kutokana na ubovu wa Barabara
Wananchi haoStephan Malimi na Bahati Ezekiel wameeleza kwa kuipongeza serikali hatua hiyo
ya ujenzi wa Barabara kilomita 9 kwa kiwango cha Lami, kwani kwa sasa yapo
mawasiliano ya karibu na haraka na maeneo ya Nyamadoke na Nyamhongolo Barabara
kuu ya Mwanza Musoma, japo ni eneo dogo lakini siku za nyuma walipata adha
kubwa
‘’Tunashukuru kwa hili jambo maana kutoka hapa hadi Igoma tulikuwa
tunatozwa shilingi 4000 mpaka tano lakini baada ya kukamilika Barabara,
tunatozwa shilingi 1500 hadi 2000 na kwa kuwa tumewekewa ata taa za Barabarani
hatuna shida hata usiku tunatembea bila wasiwasi’’amesema Malimi’’
Hata hivyo lai imetolewa kwa wananchi hao kuhakikisha miundombinu hiyo
inatunzwa ili iweze kutumika kwa muda mrefu ameeleza Meneja wa Tarura Wilaya ya Ilemela Sobe Makonyo
Aidha Mhandisi Makonyo ameongeza
kuwa Barabara hizi zinakadiliwa zitumike kwa muda wa miaka 20 na si kwamba muda huo ziwe zimeharibika
kabisa ila tu zinaweza kuwa zinafanyiwa ukarabati mdogo, zinahitajika kutumika
kwa muda mrefu huku akiwataka Wananchi kuwa watunzaji wa miundombinu hiyo
Wilaya ya Ilemela ina Mtandao wa Barabara za aina tofauti zipatazo kilomita 875 ambapo zimo za Zege, Mawe na
Vumbi, huku mtandao wa lami ukiwa ni kilomita 50 na Barabara hizo mpya, zenye urefu wa kilomita 12 hadi
kukamilika kwake zinagarimu kiasi cha 23 bilion





Maoni
Chapisha Maoni