Wadau wa Elimu kusaidia vifaa kwa Wanafunzi kuongeza chachu ya ujifunzaji


















 

 Ukosefu wa vifaa muhimu vya shule kama vile madaftari na kalamu umetajwa kuathiri pakubwa maendeleo ya wanafunzi wa shule za msingi katika Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji na kupelekea wengi kushindwa kuendelea na masomo.

Hayo yameelezwa na Afisa Elimu Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji Gaston Mwanache, wakati wa hafla ya kutoa zawadi ya vifaa vya shule kwa wanafunzi wa shule za msingi Bushabani na Kibirizi waliofanya vizuri katika masomo yao mwaka uliopita 2025.

Amesema ukosefu wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wa shule za msingi katika kata hiyo ni changamoto kubwa inayotokana na hali duni za baadhi ya familia na baadhi ya wazazi kutowajibika ipasavyo katika malezi ya watoto wao kwa kuwaacha wakilelewa na bibi zao.

Kwa upande mwingine badhi ya  walimu wa shule za msingi Bushabani na Kibirizi wamewapongeza wadau wa elimu wakiwemo Taasisi ya Kigoma Elimu Foundation kwa kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo yao, wakieleza hatua hiyo imeongeza hamasa kwa wanafunzi kusoma kwa bidii.

Walimu hao Mikidad Majojo na Yasin Bubelwa wameeleza kuwa Mwanafunzi anapokosa Mahitaji anakosa ujasili katika kujituma kufanya kazi za darasani hivyo hawa Wadau wamekuwa wakisaidia kuongeza nguvu pale wazazi wanapokuwa wameishia na pia uleta changamoto kwa wanafunzi kuongeza bidii ya ujifunzaji.

Taasisi ya Kigoma Elimu Foundation imeanza programu ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi kumi na mbili katika Manispaa ya Kigoma Ujiji miaka saba iliyopita ambapo mkurugenzi wa taasisi hiyo Anzuruni Kiroboto, amesema program hiyo imeleta mabadiliko chanya.

 

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HALMASHAURI YA KIBONDO KULIGAWA JIMBO LA MUHAMBWE

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

40 CHADEMA KIBONDO WAJIONDOA