Shukran kwa wanaosaidia katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

 

















Viongozi wa Dini ya Kiislam mkoani Kigoma wamepongeza taasisi na watu binafsi wanaojitokeza na kutoa sadaka ya Iftar kwa waislam waliofunga kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Hayo yamejiri wakati Taasisi ya The Islamic Foundation ilipotoa sadaka ya Futari pamoja na chakula cha daku, kwa waislam waliofunga katika Manispaa ya Kigoma Ujiji kama sehemu ya kuimarisha funga zao.

Viongozi hao wakiwemo Macho Hamisi Feruz, Sheikh wa Kata ya Gungu katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Sheikh Bazir Ismail, Naibu Amir Mkoa wa Kigoma Jamaat Answer Suna, wamesema hatua hiyo inawatia nguvu waislam kuendelea na funga yao kwa furaha na usalama.

Baadhi ya waislam waliopokea zawadi hizo ambazo zinajumuisha mchele, sukari, mafuta na tende, wameishukuru Taasisi ya The Islamic Foundation, na kuiombea izidi kudumu ili iweze kugusa maisha ya watu wengi zaidi katika shughuli zake za kuhudumia jamii.

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HALMASHAURI YA KIBONDO KULIGAWA JIMBO LA MUHAMBWE

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

40 CHADEMA KIBONDO WAJIONDOA