Watendaji ongezeni jitiada elimu na hamasa masuala ya Lishe

 








Tumain Munna Afisa Lishe Wilaya ya Kibondo



Halima Madenge Mshiriki



Mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Mstaafu agrey magwaza amewataka watendaji wa kata kuhakikisha wanasimamia zoezi la wazazi kuchangia chakula mashuleni Hali ambayo itaongeza hamasa ya watoto kuelewa kile wanachojifunza na kuwafanya kuwa na afya bora

Ameyasema hayo wakati wa  kujadili taarifa ya Hali ya lishe Kwa watoto katika kipindi Cha robo ya tatu ya October hadi December ambapo amesema Kila mzazi anatakiwa aone umuhimu wa kuchangia chakula kwaajili ya watoto ili waweze kufikia malengo yaliyokusudiwa

Aidha  agrey amewataka walimu kutumia maeneo ya yaliyo wazi kwaajili ya kilimo na kuzalisha chakula ambacho kitasaidia kuendelea kuboresha afya za wanafunzi Hali ambayo itasaisaidia pia kupunguza wingi wa michango ya chakula Kutoka Kwa wazazi

Fundi Hamisi Mtendaji Kata ya Kitahana na Marushwa Marushwa Mtendaji Kata ya Lugongwe wameahidi kuendelea kufanya utekelezaji hasa katika kuhamasisha na kuelimisha jamii kutambua umuhimu wa Lishe kwa Watoto na kujitoa kuchangia chakula mashuleni

‘’Japo uelewa bado ni mdogo katika jamii zetu, hali ambayo imekuwa ikipelekea wengi  kuchajali, ila tunaendelea kuwaelimisha wananchi , na hali itakuwa nzuri tu kuelekea malengo mahususi’’ amesema Hamisi

Kwa wake upande afisa lishe wilaya ya Kibondo Tumaini Muna amesema Hali ya lishe inaendelea kuimalika huku akiwaomba viongizi wa vijiji na kata kuendelea kutoa elimu Kwa wazazi kuhusu utoaji wa vyakula vyenye lishe ili kuimarisha afya ya motto

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HALMASHAURI YA KIBONDO KULIGAWA JIMBO LA MUHAMBWE

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

40 CHADEMA KIBONDO WAJIONDOA