Mabadiliko ya Ongezekola Idadi kubwa ya Wanafunzi 2027, Mikakati iongezeke ujenzi wa Miundo mbinu
Mwanza. Kutokana na
mabadiliko ya Mitaala ya Elimu katika shule za Msingi na Sekondari hapa nchini,
hatua itakayopelekea Wanafunzi wengi kumaliza elimu ya Msingi kuelekea
sekondari, serikali imeshauliwa kulitazamaa kwa jicho la pekee suala la ujenzi
na uanzishwaji wa shule za sekondari ili kuleta tija
Darasa la saba na sita ni makundi
yanayotarajiwa kumaliza elimu hiyo huku idadi ya shule na vyumba vya madarasa
vikiwa ni vichache hatua inayotajwa kuwa huenda ikakwamisha malengo mahususi
Hayo yameelezwa na Madiwani wa Halmashauri ya Magu Mkoani mwanza walipokuwa
wakijadili Bajeti ya Halmashauri hiyo ya 2026/27ambapo John Ngagaje Diwani Kata ya Shisha na Jackson
LugwishaKata ya Lutale wanasema kuwa ni vema pia bajeti hiyo ikajielekeza
kunusulu sekta ya elimu hasa kwenye miundombinu
Awali akisoma taarifa ya rasmu ya
Bajeti hiyo Afisa Mipango wa Halmashauri ya Magu Mofeni Mwakajonga amesema
Bajeti hiyo imetia hatua zote za kisheria na imezingatia Mahitaji yote huku Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Edwad Kihamba
akisema serikali inalitambua hilo na
akiendelea kusisitiza usimamizi mzuri wa vyanzo vya mapato ili kufikia malengo
‘’Upo utaratiu unaendelea wa
kuboresha miundombinu kwa kukarabati na kujenga kwanza shule zilizopo hivyo
mpango huo uttakuwa endelevu mpata hatua malengo mahususi yatakapofikiwa’’
amesema Kihamba
Sambamba na uboreshaji wa Miundombinu
ya Elimu, Watumishi wa Halmashauri pamoja na Madiwani wametakiwa kuhakikisha
wanasimamia vyema Miradi na Vyanzo vya Mapato ili bajeti yenye jumla shilingi
73 bilion ilete manufaa katika kuwahudumia wanancnhi anaeleza Diana Philemon
Makamu Mwenyeki Halmashauri ya Magu
Maoni
Chapisha Maoni