Mkoani Kigoma,Serikali ya Wadau kuendelea kuboresha huduma zaAfya
Serikali kwa kushirikiana na wadau wameendelea kupiga
hatua muhimu kuelekea kufikia malengo endelevu ya mwaka 2030 ya kupunguza vifo
vitokanavyo na uzazi kufikia vifo 70 kwa vizazi hai laki moja na vifo vya
watoto wachanga kufikia vifo 12 katika vizazi hai elfu moja.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon
Sirro, aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua kwenye
uzinduzi wa mradi wa Mjamzito na Mtoto Salama utakaotekelezwa na Shirika la
Thamini Uhai, ukilenga kuchangia katika juhudi za serikali za kupunguza vifo
vya uzazi na watoto wachanga.
Amesema hatua hizo ni pamoja na kuboresha na kuimarisha miundombinu pamoja na vifaa tiba kwenye sekta ya afya, na kwamba juhudi zinazofanywa na wadau kama vile Shirika la Thamini Uhai ni muhimu katika kufikia malengo hayo.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Joachim Masunga, amesema kupitia mradi wa Mjamzito na Mtoto Salama, utaleta tija kubwa kwenye jitihada za kupambana na vifo vitokanavyo na uzazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Thamini Uhai Banzi
Msumi, amesema mradi wa Mjamzito na Mtoto Salama ni wa miaka mitano na
utatekelezwa katika mikoa mitatu ya Kigoma, Geita na Katavi, unakwenda
kuimarisha maeneo muhimu manne ya huduma jumuishi za Mama na Mtoto.





Maoni
Chapisha Maoni