2,352 Walioacha Masomo Mkoani Kigoma kureshwa Mashuleni
![]() |
| Farida Sebalua Afisa Elimu UNICEF Kigoma |
![]() |
| Simon Siro Mkuu wa Kigoma |
Kigoma. Mkoa wa Kigoma kupitia mradi wa Elimisha Mtoto umefanikiwa kuwarejesha shuleni watoto 2,352 waliokuwa wameacha shule kupitia mfumo rasmi au nje ya mfumo rasmi.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon
Sirro, kwenye kikao cha kuendeleza kampeni ya kuhimiza uandikishaji na
kuwarejesha watoto walio nje ya shule iliyozinduliwa Desemba mwaka 2025.
Balozi Sirro, amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka
2026 bado wapo watoto wenye umri wa kati ya miaka 6 na 15 ambao
hawajaandikishwa shuleni katika mfumo rasmi au nje ya mfumo rasmi wa shule na
kwamba serikali kwa ushirikiano na Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani UNICEF
na wadau wengine inalenga kuwandikisha watoto wote ambao hawajaandikishwa na kuwarejesha
walioacha masomo kutokana na sababu mbali mbali.
Kwa upande wake Afisa Elimu kutoka UNICEF, Ofisi ya
Kigoma Farida Sebalua, amesema tafiti zinaonyesha kuwa mkoa wa Kigoma
unakabiliwa na tatizo la mdondoko huku akibainisha sababu za tatizo hilo.
Mradi wa Elimisha Mtoto unaofadhiliwa na Education
Above All, ukishirikiana na UNICEF pamoja na serikali ulianza kutekelezwa mwaka
2022 na utahitimishwa mwaka 2027, ukichangia juu ya kile ambacho serikali
ilikianzisha kwenye program ya MEMKWA.




Maoni
Chapisha Maoni