POLISI KIGOMA WAADHIMISHA WIKI YA POLISI JAMII KWA KUCHANGIA DAMU

KIBONDO.Jehi la Polisi Mkoa wa
Kigoma katika kuadhimisha wiki ya Polisi jamii, limefanya uafi na kuchangia
Damu katika hospitali ya Wilaya ya Kibondoili kusaidia kuokoa maisha ya Watu
wanaohitaji huduma hiyo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma SACP Pilmoni Makungu akiongea
na Waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo, amesemalicha ya kupunguza uhitaji
wa Damu katika vituo vya kutolea huduma za Afya,lengo kubwa ni kuonyesha
ushiriki wa Jeshi hilo katika masuala ya
Kijamii
Aidha Makungu ameongeza kuwa katika Wiki hii,zinafanyika
shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na Michezo, Usafiri na kuchangia Damu ili
kuokoa maisha ya wahitaji wa Damu
Naye Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kibondo Colnely
Livin zoezi hilo linaonyesha namna Polisi linavyoshiriki katika utoaji wa
huduma ndani ya Jamii
Jumla ya Unit 36 za Damu zimepatikana katika zoezi hilo la
uchangiaji Damu huku Jeshi hilo likiitaka jamii kuendelea kudumisha amani
ambapo Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Colnely Livin akeleza kuwa Damu hiyo
itasaidia kupunguza huitaji wa Damu
katika Hospitali hiyo na kulipongeza Jeshi hilo kwa maono hayo ya kuchangia
Damu
Kwa upande wao baadhi ya Wananchi Jonathani Ndahana na Melani
Amoni pamoja na kulipongeza Jeshi hilo la Polisi kujitoa kushiriki katika kazi
za kijamii katka maadhimisho ya Polisi ya Jamii ni vema lijenge tabia ya
kushikiana na Wananchi bila kusubili Matukio
‘’Tunalipongeza Jeshi hili kwa hatua hiyo maana tumezoea kuwa
wao wapo kwa ajiliya mambo ya ulinzi pekee kumbe hata ushiriki wa mambo
mengine unawahusu na hali hii inajenga
umoja na wananchi hata katika kudhibiti uharifu’’amesema Amosi


Maoni
Chapisha Maoni