SIKU YA HOMA YA INI

 


Kila ifikapo julai 28 kila mwaka Dunia uadhimisha siku ya homa kali ya Ini, lengo ikiwa ni kujenga uelewa kwenye jamii kuhusu tatizo hilo na namna ya kujihami na ili kuepukana na hali hiyo

Homa ya Ini ni kuvimba kwa ini. Kitendo cha ini kuvimba ghafla  ndio huitwa Homa kali ya Ini. Sababu zinazofahamika zaidi za ini kuvimba ghafla ni maambukizi ya virusi vya homa ya ini aina A na E na ni katika matukio machache sana virusi vya homa ya Ini B na C. Aina fulani za dawa za matibabu ambazo zina sumu zinaweza pia kusababisha homa Kali ya ini. Mara nyingi inaweza kupona bila hata madhara makubwa au kuhitaji matibabu lakini katika matukio machache huweza kusababisha ini kushindwa kufanya kazi na wakati mwingine kifo.

Na hizi ndizo dalili za homa kaliya Ini

Bila kujali visababishi, dalili za homa kali ya ini ni pamoja na:

-          Kutapika, kuhara au maumivu ya tumbo

-          Rangi ya manjano kwenye macho na ngozi.

-          Choo kilicho na rangi mpauko.

Kwa kawaida, homa kali ya ini inaweza kupona bila hata madhara ya hapo kwa hapo Katika baadhi ya wagonjwa, maambukizi ya homa kali ya ini aina B au C yanaweza kusababisha maambukizi sugu na kusababisha kovu, ini kushindwa kufanya kazi au hata saratani. Homa kali ya ini inakuwa mbaya zaidi kwa watu wazima kuliko watoto. Watu wazima huonesha zaidi dalili za ugonjwa kuliko watoto na madhara makubwa zaidi ya ugonjwa huo ni kwa watu wenye umri mkubwa.

Idadi kubwa ya watoto huwa hawaoneshi kabisa dalili na ni wachache sana ambao Ngozi na macho hubadilika rangi na kuwa manjano. Inaweza ikaisha haraka bila matibabu au huduma maalum, lakini kuna wakati inaweza kusabaisha ini kushindwa kufanya kazi au kifo. Kunawa mikono kunaweza kuepusha mtoto kuambukizwa homa ya ini aina A na E.

Iwapo una hofu ya kwamba mtoto wako ana dalili za homa kali ya ini, tafadhali onana na daktari ili upate ushauri wa jinsi ya kumpatia mtoto wako huduma anayohitaji

Changamoto kubwa ni jamii kutokuwa na tabia ya kupima afya ambayo husaidia kujua hali ya kiafya ya Mtu na namna ya kudhibiti au kuzuia Magonjwa,  na wengi wakiogopa garama za upimaji na hofu ya kujua hali walizonazo

Licha ya uwepo wa Dalili za Magonjwa mbalimbali ambazo uelezwa na wataalam wa huduma za afya, Watu wengi upoteza muda kwa kutumia njia za kienyeji kama dawa za mitishamba na Waganga wa kienyeji.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI SGR NA KUZINDUA MELI NNE ZA MIZIGO ZIWA TANGANYIKA

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu