Machapisho

Al Shabaab yatishia kushambulia Ulaya

Picha
Waziri wa Usalama wa Marekani anasema analitia maanani sana tishio la kundi la Waislamu wa Somalia, Al Shabaab, kwamba litashambulia maeneo ya maduka huko Marekani, Canada na Uingereza. Katika mahojiano kwenye televisheni, Jeh Johnson alisema pametokea mabadiliko katika vitisho vya makundi ya wapiganaji Waislamu ambayo sasa yanatoa wito kwa washabiki wao katika nchi maalumu kufanya mashambulio. Ulinzi umezidishwa kwenye eneo moja la maduka la Marekani katika jimbo la Minnesota, ambalo lina wakaazi wengi Wasomali Mwaka wa 2013, shambulio lilofanywa na Al Shabaab dhidi ya eneo la maduka la Westgate mjini Nairobi, Kenya, liliuwa watu zaidi ya 60.

Ukraine yaomba msaada wa ulinzi

Picha
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko, amevitaka vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani kupelekwa mashariki mwa nchi hiyo ili kuhakikisha zoezi la kusitishwa kwa mapigano linafanikiwa. Ametoa wito huo katika mkutano maalum wa dharura wa baraza la usalama, baada ya vikosi vya Ukraine kujitoa katika mji wa mashariki wa Debaltseve kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi. Pande zote mbili zimekuwa zikilaumiana kwa kukiuka makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano yaliyofikiwa wiki iliyopita. Kwa upande wake, serikali ya Marekani imesema Urusi na kundi la waasi linaloliunga mkono wameshindwa kutimiza makubaliano yaliyosainiwa wiki iliyopita na viongozi wa Ujerumani, Ukraine, Ufaransa na Urusi. Viongozi hao wanne walipanga kujadiliana kuhusu mustakbali wa eneo hilo jana usiku. Awali msemaji wa kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema makubaliano hayo yanapitia wakati mgumu.

Libya yaomba kuondolewa vikwazo

Picha
Serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha ili kukabiliana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo. Akihutubia kikao cha dharura cha baraza hilo, waziri wa mambo ya nje wa Libya,Mohammed al-Dairi amesema hatua hiyo itaisaidia serikali ya Libya kujenga jeshi lake, ili kuwatokomeza Islamic State na makundi mengine ya wapiganaji. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Libya aliungwa mkono na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry, ambaye amesema jumuia ya kimataifa inatakiwa kuisaidia serikali ya Libya ili kuonyesha mamlaka yake nchini humo. On Afisa wa Libya katika kikao cha kimataifa  Mapema wiki hii, ilithibitika kuwa wapiganaji wa Islamic State nchini Libya waliwakata vichwa mateka kutoka Misri.

Obama:Vita ni dhidi ya magaidi si Uislam

Picha
Rais Barack Obama ameliambia kongamano dhidi ya misimamo mikali ya kidini akisema kuwa kuwa wako kwenye vita si na Waislamu bali na magaidi waliouchafua Uislamu. Bwana Obama amesema ni sharti dunia ikabiliane na itikadi zilizopindishwa na makundi kama Islamic State yanayochochea vita na kuwapa vijana mafundisho yenye misimamo mikali ya imani ya kidini . Ameyasema hayo katika mkutano wa siku tatu unaofanyika mjini Washington ambapo amesema dunia inatakiwa kukabiliana na makundi ya aina hiyo. Rais Obama ameeleza kuwa manung'uniko waliyonayo vijana lazima yashughulikiwe ili kuondokana na hisia za makundi yenye misimamo mikali ya kiitikadi. Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi sitini wanahudhuria mkutano huo ambao umekuja kufuatia mashambulio ya makundi ya Kiislam katika nchi za Denmark, Ufaransa na Australia.

Majambazi yatikisa Zanzibar

Picha
Na Mwadishi Wetu, Zanzibar MAJAMBAZI yametikisa viunga vya Mtaa wa Darajani kisiwani Zanzibar na kusimamisha shughuli za biashara wakati polisi walipowakimbiza na kuamua kutumia risasi za moto. Tukio hilo lilitokea jana saa nane mchana na kusababisha watu wawili kujeruhiwa na watatu kupoteza fahamu kutokana na vishindo vya risasi na mabomu wakati majambazi hayo yalipotaka kutoroka. Taarifa zaidi zinasema gari ya majambazi hayo iliwagonga wanawake wawili baada ya kuingia kwa kasi katika eneo la wafanyabiashara wa Darajani maarufu kwa jina la Jua Kali. Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema majambazi hayo yalikuwa na gari aina ya Toyota Noah yalikimbizana na polisi na walipofika katika kituo cha zamani cha daladala walipotea njia kwa kutaka kupita kulia kabla ya gari yao haijakwama katika ukuta wa Shule ya Msingi Darajani. Mkazi wa Michenzani, Said Musa Ali, alisema wakati wakishangaa gari hiyo kuingia kwa kasi, ghafla wanawake wawili waligongwa na kusukumwa pembeni h...

Wasomali wawili mbaroni Tanga

Picha
NA WAANDISHI WETU, TANGA JESHI la Polisi nchini kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), limewatia mbaroni watuhumiwa wawili wanaodaiwa kuwa na asili ya Somalia katika msako unaoendelea dhidi ya kundi la wahalifu wa silaha mkoani Tanga. Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi mjini hapa, kiliiambia MTANZANIA kuwa watu hao walikamatwa jana saa 5 asubuhi katika eneo la Kijiji cha Amboni Mafuriko, baada ya kuonekana katika eneo hilo wakiwa wanashangaa na hawajui wanakokwenda. Baada ya kuonekana kwa watu hao, wananchi wa kijiji hicho kilicho jirani na Kijiji cha Mleni ambako kundi la wahalifu wa silaha lilijificha, walitoa taarifa kwa polisi ambao walifika na kuwatia mbaroni. “Ni kweli leo (jana) saa tano asubuhi huku eneo la Kijiji cha Amboni Mafuriko kuna watu wawili wenye asili ya Somalia walikamatwa baada ya wananchi kuwaona na kuwatilia shaka, na hivyo kufanikisha kukamatwa,” kilisema chanzo hicho. Wakati huohuo, jeshi hilo linawashikilia wat...

JK atema wakuu wa wilaya 19

Picha
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya kwa kuwateua wapya 27, huku akiwahamisha 64 katika vituo vyao na wengine 42 amewabakisha katika maeneo yao ya zamani. Akitangaza mabadiliko hayo jana mjini hapa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwapo kwa nafasi 27 zilizokuwa wazi kutokana na wakuu wake wa wilaya watatu kufariki dunia na wengine kupandishwa vyeo kuwa wakuu wa mikoa. “Wakuu wa wilaya 27 wameteuliwa kuziba nafasi zilizoachwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo wengine kufariki dunia, kupandishwa vyeo kuwa wakuu wa mikoa, kupangiwa majukumu mengine na wengine uteuzi wao kutenguliwa,” alisema Pinda. WAKUU WA WILAYA WAPYA Waziri Mkuu aliwataja wakuu wa wilaya wapya pamoja na vituo vyao vya kazi kuwa ni Mariam Mtima (Ruangwa), Dk. Jasmini Tisiike (Mpwapwa), Paloleti Mgema (Nachingwea), Fadhili Nkurlu (Misenyi), Felix Lyaniva (Rorya), Fredrick Mwakalebela (Wanging’ombe) na Zainab Mbussi (Rungwe). Wengine ni Fran...