Ukraine yaomba msaada wa ulinzi
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko,
amevitaka vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani kupelekwa
mashariki mwa nchi hiyo ili kuhakikisha zoezi la kusitishwa kwa mapigano
linafanikiwa.
Ametoa wito huo katika mkutano maalum wa dharura wa baraza la usalama, baada ya vikosi vya Ukraine kujitoa katika mji wa mashariki wa Debaltseve kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi. Pande zote mbili zimekuwa zikilaumiana kwa kukiuka makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano yaliyofikiwa wiki iliyopita.
Kwa upande wake, serikali ya Marekani imesema Urusi na kundi la waasi linaloliunga mkono wameshindwa kutimiza makubaliano yaliyosainiwa wiki iliyopita na viongozi wa Ujerumani, Ukraine, Ufaransa na Urusi.
Viongozi hao wanne walipanga kujadiliana kuhusu mustakbali wa eneo hilo jana usiku.
Awali msemaji wa kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema makubaliano hayo yanapitia wakati mgumu.
Maoni
Chapisha Maoni