Libya yaomba kuondolewa vikwazo
Serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa imeliomba Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa kuiondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha ili
kukabiliana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.
Akihutubia kikao cha dharura cha baraza hilo, waziri wa mambo ya nje wa Libya,Mohammed al-Dairi amesema hatua hiyo itaisaidia serikali ya Libya kujenga jeshi lake, ili kuwatokomeza Islamic State na makundi mengine ya wapiganaji.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Libya aliungwa mkono na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry, ambaye amesema jumuia ya kimataifa inatakiwa kuisaidia serikali ya Libya ili kuonyesha mamlaka yake nchini humo.
Mapema wiki hii, ilithibitika kuwa wapiganaji wa Islamic State nchini Libya waliwakata vichwa mateka kutoka Misri.
Akihutubia kikao cha dharura cha baraza hilo, waziri wa mambo ya nje wa Libya,Mohammed al-Dairi amesema hatua hiyo itaisaidia serikali ya Libya kujenga jeshi lake, ili kuwatokomeza Islamic State na makundi mengine ya wapiganaji.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Libya aliungwa mkono na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry, ambaye amesema jumuia ya kimataifa inatakiwa kuisaidia serikali ya Libya ili kuonyesha mamlaka yake nchini humo.
On |
Maoni
Chapisha Maoni