Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2015

Kakonko yapitisha Rasmu ya bajeti Bilion 26 mwaka 2015/16

Picha
Mwemezi Muhingo Mwananchi Katika mwaka wa fedha wa 2015/16 Halamashauri ya wilaya kakonko Mkoani imepanga kukusanya na kutumia jula ya  Tsh Bilion 26.4kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo ruzuku ya serikali kuu bilion 25 na mapato ya ndani tsh milion 436 ambapopo mchango wa serikali kuu ni sawana asilimia 98.3 ya bajet ya Halmashauri Akisoma taarifa yake wakatati wa kikao cha Baraza la madiwani kilifanyika mjini kakonko  kwa ajili ya kujadili mipango na Rasimu ya mapendekezo ya Bajeti ya Halmashauri hiyo, kwa mwaka wa fedha wa 2015/16  Bw, Galpa Sedoyeka, amesema kuwa vipaumbele vya bajeti hiyo nikujikita zaidi katika mswala ya elimu Sedoyeka amesema kuwa mpango wa mwaka 2015/16  umeandaliwa kwa kuzingatia vipaumbele na kiutekelezaji  kuboresha utoaji elimu bora ili kuongeza kiwango cha ufaulu kuwaandaa wanafunzi kuweza kukabiliana na na maisha baada ya kumaliza masomo Hata hivyo ametaja vipaumbele vingine kujenga Ofisi za Halmashauri ujenzi wa nyumb...

Watu wane wa Familia moja wafariki baada ya chakula chenye sumu

Picha
Watu wane wa Familia moja wafariki baada ya chakula chenye sumu Mwemezi Muhingo Kakonko Watu wanne wa Familia moja wakazi wa kijiji cha Kibambila wilani Kakonko mkoa wa Kigma wamefariki dunia baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana wilayani hapo kwa kuwahusisha watu watano ambapo wanne walifariki dunia na mmoja kunurika kifo na baadae kuruhusiwa kwenda nyumbani Mganga  aliyekuwa zamu katika kituo cha Afya cha kakonko ambacho kinatumika kama Hospitali ya wilaya  Bi, Ndalikunda Kweka, amesema kuwa watu hao walifikishwa hospitalini hapo baadhi yao   wakiwa na hali mbaya ila kadri muda ulivyokuwa ukisogea ndipo walipokuwa wakiziwa na wengine kupoteza maisha. Nae Mganga mkuu wa wilaya hiyo Bw  Fadhili Seleman amesemakuwa kuwa mara baada ya wagonjwa hao kufikishwa hospitalini hapo walipowafanyia uchunguzi waligundua kuwa wamekula vitu vyenye sumu na baada ya kuhoji kwa waliokuwa na fahamu...

Watumia zaidi ya masaa sita kutafuta Maji

Picha
Watumia zaidi ya masaa sita kutafuta Maji Muhingo Mwemezi Mwananchi Baadhi ya wananchi wa kijiji cha kigendeka kata ya busagara wilayani kibondo mkoani kigoma wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji hali inayo walazimu kutumia zaidi ya masaa sita wakitafuta huduma ya maji huku wakikwama katika shughuli nyingine za  kimaendeleo. Wakizungumza na gazeti la mwananchi wakazi ambao ni Jahson Kabuka na Zabron Reuben wamedai kuwa kijiji hicho kina kisima kimoja baada ya visima vinne kuharibika na hata kilichopo kinatoa maji kidogo sana na kwakuwa kijiji kina idadi ya watu 9800 ambapo hupelekea mrundikano wa watu katika kisima hicho na kuzua fujo zisizo kuwa na msingi huku baadhi yao wakitoleana matusi na kugombana hali inayo hatalisha usalama wao. Nae  mmoja wa wakazi hao bi Helen Kavula .amesema hata hivyo kutokana na mda mwingi wanao tumia katika kutafuta maji,  kumepelekea kuwepo kwa kukwama kwa shughuli za kijamii katika utafutaji wa mahitaji ya kifam...

Mtendaji wa kata akataliwa, wakijiji afukuzwa kazi katika mkutano wa hadhara

Picha
Mtendaji wa kata akataliwa, wakijiji afukuzwa kazi  katika mkutano wa hadhara Wananchi wa Kijiji cha kigendeka Kata ya Busagara wilayani kibondo mkoa wa kigoma wamemmfukuza kazi Mtendaji wa kijiji, kukataa kufanyakazi na mtendaji wa Kata kwenye mkutano mkuu uliofanyika kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo,  kwa madai kuwa wote wawili walishirikiana kugushi mhuri wa ofisi ya kijiji na kugawa ardhi hekali 100 kinyume cha taratibu Uamuzi wa  wakazi hao umefikiwa baada kikako cha  uongozi wa kijiji hicho kilichokaa Tarehe 15.1.2015 baada ya kubaini matatizo hayo, na kumuita mtendaji huyo na kumueleza makosa yake  hali iliyowafanya wajumbe wa kikao hicho kutokuwa na Imani nae na kumtaka aachie ngazi hatua iliyofikia mwenyekiti Bw, Yotham Kitwe  kuitisha mkutano mkuu wa kijiji ili kutoa maamuzi.   Awali mkutanoni hapo, ilidaiwa kuwa mwaka jana tar 24.4.2014 Bw Abeli Fransisco akiwa ni mwenyekiti wa kitongoji, aliiba mhuri wa Afisa mtendaji w...

Dc awataka Viongozi wote serikali za mitaa waliochaguliwa hivi karibuni kutimiza wajibu wao kila mmoja na kuondoa tofauti za vyama

Picha
Kibondo;  Mkuu wa wilaya ya Kibondo mkoani kigoma bw. Venance Mwamoto amewata viongozi waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mapema mwaka jana kufanya kazi kwa bidii katika kuchochea maendeleo ya wilaya. Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na viongozi hao katika Tarafa ya mabamba kata ya mabamba mara baada ya kuapa kulitumikia taifa na wananci kwa moyo mmoja na ushilikiano katika kudhibiti matukio machafu. Bw.mwamoto amesema katika utawala wa serikali ngazi ya chini ni kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa na hivyo wao wanapaswa kluwa chachu ya kuchochea maendeleo ikiwa ni pamoja  na kutoa taarifa juu ya uharifu. Mwamoto alisema kuwa uongozi ngazi ya vitongoji ni  hatua muhimu sana kwani hakuna serikali kuu bila kuanzia ngazi ya kitongoji hivyo ni vyema viongozi hao wajiamini na kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana ili kufikia mafanikio. Aidha aliwataka kuachana tabia ya mashindano ya kisiasa  ambayo kwa sasa hayawez...

Wampinga Kabila kuwania urais nchini DRC

Picha
Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamewafyatulia risasi waandamanaji kwenye mji mkuu Kinshasa walio na hasira katika kile kinachoonekana kama jitihada za kutaka kuongoza uongozi wa rais Joseph Kabila. Watu kadha walitolewa eneo la kati kati mwa mji wakiwa na majeraha ya risasi ambapo pia kulitoka makabiliano kwenye chuo kikuu cha mji huo. Milio ya risasi iliripotiwa katika maandamano mengine katika mji ulio mashariki wa Goma. Watu kadhaa walipatikana na majeruhi ya risasi katikati mwa mji huo huku ghasia zengine zikiripotiwa katika katika chuo kimoja kikuu. Viongozi wa upinzani waliitisha maandamano hayo baada ya bunge dogo kuidhinisha sheria siku ya jumamosi inayoagiza kufanyika kwa hesabu ya idadi ya watu kabla ya uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka ujao. Wabunge hao wa upinzani wamesema kuwa mpango huo utachelewesha uchaguzi huo ambao umekuwa ukingojwa kwa hamu kwa miaka kadhaa. Rais Joseph Kabila ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 15 amehudumu miula miwili ...

Mafuriko yawaua watu 200 Malawi

Picha
Watu 200 waaga dunia kutokana na mafuriko Malawi Utawala nchini Malawi unasema kuwa umewaokoa maelfu ya watu ambao walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko ambayo yameikumba nchi hiyo. Wanajeshi walitumia mashua na ndege za helikopta kuwahamisha watu kwenda maeneo yaliyoinuka kufuatia kuharibiwa kwa barabara na madaraja. Takriban watu 200 wameripotiwa kuaga dunia huku wengine 200,000 wakilazimika kuhama makwao. Serikali ya msumbiji imeomba msaada wa kimataifa ambapo pia imeweka kambi ikiwa inawapa waathira chakula maji na makao.

Wanafunzi wapinga unyakuzi wa ardhi Kenya

Picha
Polisi nchinikenya katiika mji mkuu Nairobi leo imewafyetulia gesi ya kutoa machozi wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa ardhi waliyokuwa wanatumia kama kiwanja cha kuchezea na mmiliki binafsi. Polisi hao wakiwa na Mbwa waliwatawanyta wanafunzi hao, baadhi yao wakisemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka sita baada ya kuuangusha ukuta mpya uliojengwa kati ya shule yao na uwanja huo. Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni Lang'ata baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma walipopata kiwanja chao kikiwa kimeuzwa na hata kuwekwa uzio. Shule hio ina karibu watoto 1,000 walo kati ya umri wa miaka mitatu na kumi na minne na inasimamiwa na baraza la jiji. Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa katika purukushani hilo wakati polisi walipoingilia kati na kujaribu kuwatawanya wanafunzi hao waliokuwa wanazua rabsha. Baadhi yao walipelekewa hospitalini baada ya kupata majeraha madogomadogo. Baadhi ya wanafunzi hao walikabiliana na polisi wak...

Zitambueni kaya maskini Kwa uaminifu

 Mwemezi Muhingo Mwananchi   Meneja uhawishaji fedha kupitia mfuko wa jamii (TASAF)kutoka makao makuu  Bw.Omary malilwa ambaye alimwakilisha mkurugenzi mkuu Tasaf amewataka viongozi watakao pewa nafasi ya kufatilia kaya maskini katika wilaya ya kakonko mkoani kigoma  kuorodhesha kaya hizo bila kuwepo ubaguzi na kuwa waaminifu katika kazi hiyo. Kauli hiyo allitoa jana wakati wa kikao kilicho wakutanisha madiwani na viongozi mbalimbali wa serikali  ikiwa ni kwa awamu ya tatu kufanyika wilayani humu kwa lengo la  kunusuru kaya maskini katika nyanja mablimbali ikiwa ni pamoja na elimu,afya,hususa kwa wale ambao hawana uwezo wa kumudu ghalama hizo. Bw.Malilwa amesema mara nyingi fulsa kama hizi zinapo anzishwa huingiliwa na wanasiasa kwa kutaka kujipatia umarufu na kuvuruga mpango uliokusudiwa na serikali  na hivyo amewataka wanansiasa kutotumia nafasi hiyo kwani mfuko wa jamii haubagui chama,kabila au dini ya mtu.  Jumla ya kaya 920,0...

Madiwani Kibondo wawataka wakuu wa Idara kuwa wabunifu na waadilifu

Picha
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya  ya Kibondo mkoani Kigoma wamewalalamikia Wataalam na wakuu wa Idara za Halmashauri hiyo kwakuonyesha uwezo mdogo au kufanya makusudi kutoibua vyanzo vya mapato  hali inayosababisha  kukosekana kwa mapato na kurudisha nyuma  maendeleo. hayo yamebainishwa  na madiwani hao wakati wa kikao cha kujadili na kupitisha Bajeti ya fedha katika mwaka 2015/2016  kilichofanyikia mjini Kibondo wakidai kuwa vipo baadhi ya vyanzo ambavyo vipo na vinaonekana lakini katika taarifa havionekani hatua walio itaja kuwa ni kutaka kufanya ufisadi. Diwani wa kata ya Busagara Bw Godwini Sibanilo, amemesema vipo vyanzo vingi ambavyo katika taarifa havikutajwa na huku kila siku watu wanatozwa pesa na Halmashauri hiyo ikiwa baadhi ya vyoo vilivyoko katika maeneo mengi ya mji wa kibondo baadhi ya daiwani wakiwa kwenye kikao kwa ajili ya kujadili Bajeti ya wilwyw hiyo 2015/2016 Aidha Madiwani hao wamesema kuwa kuna miradi ambayo i...

Kanisa la teketezwa kwa Moto

Picha
Kanisa la teketezwa kwa Moto Mabaki ya kanisa la TAG lililochomwa moto Kanisa la Tanzania Assemblies of God TAG lililoko katika kijiji cha Bunyambo wilayani kibondo mkoani kigoma limeteketea baada ya kuchomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia     jumamosi ya wiki iliyopita tukio hilo likihusishwa na maswala ya kisiasa za kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mapema mwezi decemba mwaka jana   Tukio hilo lilitukia usiku wa kuamkia jumapili iliyopita majira ya saa tano usiku ambapo watu wasiojulikana waliingia kanisani hapo na kupanga thamani zote za ndani ambazo zimekuwa zikitumika wakati wa ibada na kuzimwagia mafuta ya Petrol hali iliyosababisha jingo zima kushika moto Akiongea na Clouds tv katibu wa kanisa hilo Bw Samweli Butelanya amesema kuwa tukio hilo japo hawajafahamu chanzo nini ila wao wanalihusisha na mambo ya kisiasa kwani baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa ndipo mambo hayo yametokea na kudai kuwa siku mbili...

Vitendo vya unyanyasaji kwa Walemavu

Vitendo vya unyanyasaji kwa Walemavu Pamoja na jamii kupiga vita unyanyasaji walemavu bado watu wengine wanaendeleza tabia hizo ambazo ni ukikwaji wa haki za Binadamu kwa kundi hilo , baada ya mkazi mmoja wa kijiji cha Buyenzi Kata ya Itaba Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma Bw,  Alcado Poul  kumpiga mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Alfred Jonas  ambaye  ni ulemavu na kumvunja mguu. Tukio hilo lilitukia Desemba 31 mwaka jana  majira ya saa  kumi join wakati Bw, Alfred Jonas alipokuwa anaenda sokoni kutafutaji yake ndipo alipokutana na Bw, Alcado Poul ambaye alimshika na kumnyanyua juu kasha kumtupa chini mara mbili hali iliyo msababishia majeraa na amumivu makali hatua iliyopelekea  kulazwa katika Hospitali ya wilaya ya kibondo. Kutokana na kuumia vibaya mguu kwa kuvunjika, mlemavu huyo amepewa rufaa kwenda Hospital ya Bugandondo jijini mwanza baada ya madaktari Wilayani kibondo kushindwa kumtibu kutokana na ukubwa wa tatizo ...

Kanisa la teketezwa kwa Moto

Picha
Mabaki ya kanisa la TAG lilichomwa moto Kanisa la teketezwa kwa Moto Mwemezi Muhingo Kibondo Kanisa la Tanzania Assemblies of God TAG lililoko katika kijiji cha Bunyambo wilayani kibondo mkoani kigoma limeteketea baada ya kuchomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia     jumamosi ya wiki iliyopita tukio hilo likihusishwa na maswala ya kisiasa za kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mapema mwezi decemba mwaka jana   Tukio hilo lilitukia usiku wa kuamkia jumapili iliyopita majira ya saa tano usiku ambapo watu wasiojulikana waliingia kanisani hapo na kupanga thamani zote za ndani ambazo zimekuwa zikitumika wakati wa ibada na kuzimwagia mafuta ya Petrol hali iliyosababisha jingo zima kushika moto Akiongea na Clouds tv katibu wa kanisa hilo Bw Samweli Butelanya amesema kuwa tukio hilo japo hawajafahamu chanzo nini ila wao wanalihusisha na mambo ya kisiasa kwani baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa ndipo mambo hayo yam...

Wakataeni wanasiasa Mchwala

Picha
Wakataeni wanasiasa Mchwala Mwemezi Muhingo Mwananchi Kasulu; Watanzania wametakiwa kukataa kufuata itikadi za wanasiasa wasiokuwa na maadli na uzalendo kwa kusababisha migongano na uchonganishi katika jamii kwa ajili ya kutafuta umaalufu. Hayo   yalisesemwa na mkuu wa wilaya ya Kasulu mkoani kigoma Dany Makanga, wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi, katika kikosi cha 825 kj, Mtabila Jkt kwa vijana mujibu wa sheria awamu ya pili mwishoni mwa wiki. Makanga aliwambia mamia ya wakazi wa wilaya hiyo waliohudhulia katika mahafali hayo, kuwa kumekuwepo na tabia za baadhi ya wanasiasa wanaoeneza chuki, katika jamii ili watu walichukie kundi frani na kuwalagai kuwa matatizo yao, wao wanaweza kuwasaidia hali inayoweza kuvuluga amani. Aidha alisema kuwa wananchi wengi wanaoishi kwenye vijiji vinavyopakana na kikosi cha jeshi cha mtabila jkt, kwa muda murefu wamekuwa wakiyumbishwa na baadhi ya watu kuwa maeneo hayo ni mali ya wanavijiji hivyo, na k...