Madiwani Kibondo wawataka wakuu wa Idara kuwa wabunifu na waadilifu
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wamewalalamikia
Wataalam na wakuu wa Idara za Halmashauri hiyo kwakuonyesha uwezo mdogo au
kufanya makusudi kutoibua vyanzo vya mapato
hali inayosababisha kukosekana
kwa mapato na kurudisha nyuma maendeleo.
hayo yamebainishwa na
madiwani hao wakati wa kikao cha kujadili na kupitisha Bajeti ya fedha katika
mwaka 2015/2016 kilichofanyikia mjini
Kibondo wakidai kuwa vipo baadhi ya vyanzo ambavyo vipo na vinaonekana lakini
katika taarifa havionekani hatua walio itaja kuwa ni kutaka kufanya ufisadi.
Diwani wa kata ya Busagara Bw Godwini Sibanilo, amemesema
vipo vyanzo vingi ambavyo katika taarifa havikutajwa na huku kila siku watu
wanatozwa pesa na Halmashauri hiyo ikiwa baadhi ya vyoo vilivyoko katika maeneo
mengi ya mji wa kibondo
baadhi ya daiwani wakiwa kwenye kikao kwa ajili ya kujadili Bajeti ya wilwyw hiyo 2015/2016 |
Aidha Madiwani hao wamesema kuwa kuna
miradi ambayo inajtngewa fedha zisizo kidhi mahitaji hasa kama miradi ya ujenzi
kama zahanati ya kijiji cha Bitare iliengewa fedha
kiasi cha sh. milon kumi na tano hali
ambayo inasababisha miradi mingi kubakia viporo kila mwaka na kuwaacha wananchi
wakinung’nika kwa kutopatiwa huduma stahiki.
Hadija Mauldi Diwani viti maalum kibondo mjini |
Benard Andrea Diwani kata ya Misezero |
Wakuu wa idara Halmasahauri wilaya ya kibondo |
Insert Benard Andrea Diwani kata ya
Misezero
Que in……..
Akijibu malalamiko ya madiwani hao Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo bw Judathadius Mboya , amesema sababu
inayofanya baadhi ya vyanzo vingine visitajwe ni kwasababu vingine ni vidogo na
kulingana na uingizaji wake kuwa mdogo inalazimika kuwatumia wale wanaokusanya
mapato katika vyanzo vikubwa , kwakuwa anapoajiriwa mtu anatakiwa alipwe kima
cha chini cha mshahara tsh 200,000/ wakati yeye anakusanya pesa ambazo ni
kidogo.
Hata hivyo Baraza hilo limepitisha Bajeti ya Shilingi
billion 42 ambayo itajikita katika miradi ya maenedeleo katika mwaka 2015/16
katika utekelezaji wa ,miradi mbalimbali ndani ya wilaya hiyo.
Aidha wameiomba serikali kuleta pesa
mapema ambazo zinakuwa zimeombwa kupitia kwenye bajeti husika ili kutimiza
malengo kwakuwa hata pesa za bajeti iliyopita wa pesa zilizofika ni asilimia 7 tu hali ambayo inakwamisha juhudi za kuleta maendeleo
kwa wananchi .
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw, Emili Mpfanye amewataka
madiwani hao kuwa waaminifu katika kusimaia miradi ya maendeleo kwa kuwatumikia
wananchi wao waliowaweka madarakani ili
kuondoa malalamiko huku wakitambua kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu
Pamoja na mambo mengine baadhi ya wananchi wameukosoa
utaratibu wa mchakato kutengeneza bajeti hiyo haukuzingatia ushirikiwaji wao
ili nao watoe vipaumbele vyao juu ya mambo wanayoyahitaji katika maeneo yao bali ni watu wachache
ambao hukaa na kupanga badala ya kuanzia kwenye vitongoji na kuja ngazi za
vijiji hadi kata .
Maoni
Chapisha Maoni