Kanisa la teketezwa kwa Moto
Mabaki ya kanisa la TAG lilichomwa moto |
Kanisa la teketezwa
kwa Moto
Mwemezi Muhingo
Kibondo
Kanisa la Tanzania
Assemblies of God TAG lililoko katika kijiji cha Bunyambo wilayani kibondo
mkoani kigoma limeteketea baada ya kuchomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa
kuamkia jumamosi ya wiki iliyopita tukio hilo likihusishwa na
maswala ya kisiasa za kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika
mapema mwezi decemba mwaka jana
Tukio hilo
lilitukia usiku wa kuamkia jumapili iliyopita majira ya saa tano usiku ambapo
watu wasiojulikana waliingia kanisani hapo na kupanga thamani zote za ndani
ambazo zimekuwa zikitumika wakati wa ibada na kuzimwagia mafuta ya Petrol hali
iliyosababisha jingo zima kushika moto
Akiongea na Clouds tv katibu wa kanisa hilo Bw Samweli Butelanya
amesema kuwa tukio hilo japo hawajafahamu chanzo nini ila wao wanalihusisha na
mambo ya kisiasa kwani baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa ndipo mambo hayo
yametokea na kudai kuwa siku mbili kabla kanisa la Evergelist Asemblies of God
Tanzania EAGT lililoko kijijini hapo watu wasiojulikana walibomoa jingo lanisa
hilo na kuvunja vyombo vya muziki
Hata hivyo waumini wa kanisa hilo, ambao hawakutaka kurekodiwa
waliiambia clouds kuwa swala hilo
linausishwa na mabo ya kisiasa kwa kuwa badaada ya uchaguzi wa serikali za
mitaa uliofanyika hivi karibuni Desemba mwaka jana kulianza kutokea malalamiko
miongoni mwa wanakijiji kuwa kanisa hilo lilichangia kupatikana kwa ushindi wa
mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Danford Mushachi kwani hata vyombo vya muziki
ndivyovilikuwavikitumika kufanya kampeni kwani wajumbe na mwenyekiti mwenyewe wanasali
katika kanisa hilo
Kufuatia tukio hilo mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya
kibondo bw Venance Mwamoto alifika kwenye eneo la tukio akiwa viongozi wa
kamati hiyo, ili kuona hali halisi ilivyo katika kanisa hilo ambapoaliwambia waumini hao kuwa kitendo
hicho sikizuri katika jamii na kuahidi kuwa mahakamani wote watakao
Aidha bw Mwamoto aliwataka
waumini wa kanisa hilo na jamii kwa ujumla kuacha tabia ya kuingiza siasa
katika nyumba za ibada hali inayoweza kuleta machafuko makubwa hapa nchini na kuwakataa na kuwatolea taarifa
wale wote wanaotaka kuwagawa watanzania kwa kutumia siasa nda yadini kwakuwa nyumba za ibada ni
sehemu ya kuubiri Amani.
Nao baadhi ya viongozi Dini wilayani kibondo wameeleza kushangazwa
kwao na vurugu hizo za kuchoma nyumba za ibada ni kwasababu hofu ya Mungu
miongoni mwa jamii imetoweka kama anavoeleza Dr Themeo Ndenza Askofu wa kanisa la
Anglikana Dayosesi ya Kibondo
Aidha Ndenza ameitaka jamii kuwa sheria na na taratibu za nchi haziruhusu vitendo vya
aina hiyo kwani kumshinda mtu katika ushindani wa kisiasa si sa babu ya
kuharibu mali za watu na kuitaka serikali kuwa macho kwani vitendo hivyo vya
watu kuwa jeruhi viongozi wa dini kuwauwa na kuhabu mali vinaonekana kushika
kasi huku serikali imekaa kimya hali inayoweza kuleta madhala katika jamii
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa kibondo ambao ni tamasha kikoti na Amani James wamekuwa na haya ya kusema juu
vurugu zinazotokea na kuziusisha nyumba za ibada kuwa ni vitendo vya uvunjifu wa amani kwani Dini ni taasisi ambazo zinategemewa juu ya kuleta amani katika nchi na jamaii kwa ujumla sasa kama waumini wenyewe wameanza kuchoma maeneo ambayo ni makimbilio itakuwaje?
Hata hivyo imetajwa kuwa katika sakata la uchaguzi wa serikali za
mitaa ushindani uliokuwepo ni watu wawili ambao walikuwa wagombea kupitia vyama
tofauti chadema na Ccm na wote wanasali katika makanisa tofauti EAGT na TAG
kijijini hapo ambapo alishinda mtu wa chadema katika nafasi ya mwenyekiti wa
kijiji
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni