Vitendo vya unyanyasaji kwa Walemavu
Vitendo vya unyanyasaji kwa Walemavu
Pamoja
na jamii kupiga vita unyanyasaji walemavu bado watu wengine wanaendeleza tabia
hizo ambazo ni ukikwaji wa haki za Binadamu kwa kundi hilo , baada ya mkazi mmoja wa kijiji cha
Buyenzi Kata ya Itaba Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma Bw,
Alcado
Poul kumpiga mtu mmoja aliyefahamika kwa
jina la Alfred Jonas ambaye ni ulemavu na kumvunja mguu.
Tukio
hilo lilitukia Desemba 31 mwaka jana
majira ya saa kumi join wakati
Bw, Alfred Jonas alipokuwa anaenda sokoni kutafutaji yake ndipo alipokutana na
Bw, Alcado Poul ambaye alimshika na kumnyanyua juu kasha kumtupa chini mara
mbili hali iliyo msababishia majeraa na amumivu makali hatua iliyopelekea kulazwa katika Hospitali ya wilaya ya
kibondo.
Kutokana
na kuumia vibaya mguu kwa kuvunjika, mlemavu huyo amepewa rufaa kwenda Hospital
ya Bugandondo jijini mwanza baada ya madaktari Wilayani kibondo kushindwa
kumtibu kutokana na ukubwa wa tatizo
Bw
Alfred Jonas Akiwa amelazwa hospitalini, anaeleza mkasa kamili ulivyo mkuta
hadi kujikuta anafikishwa
Hospital bila kutarajia
Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye ulemavu chawata wilayani kibondo bw.Everlisto Ngalama amewataka wananchi
kuwatambua walemavu kama watu wengine na
kuepuka kutowatende vitendo vya
kikatili.
Ngarama
amesema kuwa.kutokana na kuwepo kwa vya unyanyasaji unyanyasaji dhidi ya
walemavu hali inayo wafanya kujihihisi kama
waliotengwa na jamii na kuishi kwa hofu.
Aidha
Ngarama amesma kuwa Mtu huyo aspokatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria
chama chake kitaitisha maandamano ya walemavu ili kudai haki zao kwakuwa mambo
haya yamekuwa yakifumbiwa macho hatua inayoendelea kuchochea huku walemavu
wakijihisi kuwa wao si kama Binadamu
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi ambao ni Shida Maxmilian na Jumanne Jacobo, toka
kijijini hapo, wameeleza kusikitishwa kwa na kitendo alichofanyiwa mlemavu huyo
na kusema kuwa ni vitendo vya kikatili na kuiomba serikali kukemea vikali watu
wanao waonea wenzao bila utaratibu huku wakijua matatizo waliyonayo
Wananchi
hao wameendelea kuushutumu uongozi wa kijiji hicho kwa kufumbia macho vitendo
vya uharifu hali inayowatia hofu kwakuwa mtu yeyote anaweza kufanya jambo bila
kuogopa lolote kama anaweza kutiwa nguni, na
kudai kuwa hadi sasa mtu anaehusika kumuumiza
mlemavu huyo bado hajakamatwa
Hata
hivyo, mtendaji wa kijiji cha bunyezi bw.laurenti mahwela amesema serikali ya
kijiji kwa kushilikiana na wananchi wananendelea kumtafuta mhusika wa kitendo
hicho ili achukuliwe hatua za kisheria.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni