Wakataeni wanasiasa Mchwala
Wakataeni wanasiasa
Mchwala
Mwemezi Muhingo
Mwananchi
Kasulu; Watanzania wametakiwa kukataa kufuata itikadi za
wanasiasa wasiokuwa na maadli na uzalendo kwa kusababisha migongano na
uchonganishi katika jamii kwa ajili ya kutafuta umaalufu.
Hayo yalisesemwa
na mkuu wa wilaya ya Kasulu mkoani kigoma Dany Makanga, wakati wa kufunga
mafunzo ya awali ya kijeshi, katika kikosi cha 825 kj, Mtabila Jkt kwa vijana
mujibu wa sheria awamu ya pili mwishoni mwa wiki.
Makanga aliwambia mamia ya wakazi wa wilaya hiyo waliohudhulia
katika mahafali hayo, kuwa kumekuwepo na tabia za baadhi ya wanasiasa wanaoeneza
chuki, katika jamii ili watu walichukie kundi frani na kuwalagai kuwa matatizo yao, wao wanaweza
kuwasaidia hali inayoweza kuvuluga amani.
Aidha alisema kuwa wananchi wengi wanaoishi kwenye vijiji
vinavyopakana na kikosi cha jeshi cha mtabila jkt, kwa muda murefu wamekuwa
wakiyumbishwa na baadhi ya watu kuwa maeneo hayo ni mali ya wanavijiji hivyo,
na kudai kuwa mipika ya kikosi na vijiji haifuatwi na kuwambia kuwa wanaingiliwa
kwenye mashamba yao na kuwa wananyanyaswa kwa kutolewa katika maeneo ya
kendeshea shughuli za kilimo.
Eneo la Mtabila maali kilipo kikosi hicho, hapo mwanzo
ilikuwa ni kambi ya wakimbizi toka nchini Burundi
waliokimbia machafuko , na baada ya Warundi hao kurejea kwenye nchi yao, serikali ya Tanzania
iliamua kubadilisha matumizi kwa kuweka jeshi eneo hilo.
Hata hivyo alisema kuwa
eneo hilo lilipokuwalinatumiwa na wakimbizi chini ya shirika la umoja wa
mataifa, la kuhudumia wakimbizi mipaka ilikuwa kama ilivyo hivi sasa na
watanzania ambao ni jirani waliyatumia maeneo hayo kwashughuli za kilimo na
nyinginezoila ila baada ya kubadilisha matumizi, kwakuweka kikosi cha jeshi,
lazima taratibu zifuatwe ili kuondoa mkanganyiko.
Aidha alidai kuwa kuwa kikosi hicho kwa hivi sasa
kinaanza kuleleta wataalam wa kada mbalimbali kam kilimo Walimu, Madakitari, pia kitakuwa na nyenzo za kufanyia
kazi hivyo wananchi watanufaika na uwepo wa kikosi hicho iwapo kama watakuwa
ayari kwa kushikiana na kuhitaji msahada na ushauri kutoka kwenye taasisi
hiyo,
Kikosi hicho cha Mtabila jkt, kinapakana na vijiji vya Mugombe, Kitagata, Nyachenda,
Kinazi na wannchi wa vijiji vyote hivyo walilazimika kuacha kuendesha shuguli
za kilimo kwakuwa hivisasa jeshi linatumia kwa kazi zake.
Pamoja na mambo mengine wakatiwa kufunga mafunzo hayo ya
kijeshi, mkuu wa mkoa wa kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya,ambaye
alikuwa mgeni rasmi, aliwataka wahitimu kuwa waadilifu na kuishi kwa kufuata
maadili na taratibu za nchi kuokana na mafunzo waliyoyapata kwa kufuata kiapo
walichoapa
Machibya alisema kuwa lengo la kuanzisha jeshi la kujenga
Taifa ni kuwajenga vijana katika uzalendo wa kuipenda nchi yao, kuwa na nidhamu katika jamii, udugu na
mshikamano, hivyo vijana wote wanatakiwa kukumbuka hayo yote kwa kuytimiza.
Vijana waliomaliza mafunzo ya kijeshi kwa mujibu sheria
kikosini hapo idadi ya ni elfu 1
miamoja1na kumi toka vyuo mbalimbali vya
ualimu na waliomaliza kidato cha sita katika shule za sekondari ikiwa wavulana mia 7 hamsini na 5 na
wasichana mia 3 hamsini na 5 Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni