Watu wane wa Familia moja wafariki baada ya chakula chenye sumu
Watu wane wa Familia moja wafariki
baada ya chakula chenye sumu
Mwemezi Muhingo Kakonko
Watu wanne wa Familia moja wakazi wa kijiji cha
Kibambila wilani Kakonko mkoa wa Kigma wamefariki dunia baada ya kula chakula
kinachosadikiwa kuwa na sumu
Tukio hilo
la kusikitisha lilitokea jana wilayani hapo kwa kuwahusisha watu watano ambapo
wanne walifariki dunia na mmoja kunurika kifo na baadae kuruhusiwa kwenda
nyumbani
Mganga aliyekuwa
zamu katika kituo cha Afya cha kakonko ambacho kinatumika kama Hospitali ya
wilaya Bi, Ndalikunda Kweka, amesema
kuwa watu hao walifikishwa hospitalini hapo baadhi yao wakiwa na hali mbaya ila kadri muda
ulivyokuwa ukisogea ndipo walipokuwa wakiziwa na wengine kupoteza maisha.
Nae Mganga mkuu wa wilaya hiyo Bw Fadhili Seleman amesemakuwa kuwa mara baada
ya wagonjwa hao kufikishwa hospitalini hapo walipowafanyia uchunguzi waligundua
kuwa wamekula vitu vyenye sumu na baada ya kuhoji kwa waliokuwa na fahamu walisema
kuwa wamekula ugali. na kuwataja majina ya waliokufa kuwa ni Neema Joseph,miaka
12 Jonas Joseph18 Yusuph Joseph na Majaliwa Joseph miaka 11 aliyefariki baadaye
Aidha Dr Fadhili ameitaka jamii kuwa ni vizuri mtu
kufika haraka hosptali au kwenye kituo cha afya mara baada ya kumaliza kula
chakula ili kama kuna tatizo kubwa liweze
kuangaliwa kuliko kukaa kimya baadae kupata madhala makubwa kwa kuwa zipo sumu
ambazo zinachukuwa muda murefu kuleta madhala katika mwili wa binadamu
Baba mzazi wa Vijana waliokufa kwa sumu Bw, Joseph
Kajolo, yeye alinusurika kwakuwa hakula chakula hicho, maana alishindwa kula
kwasababu ya kuwa amelewa baada ya kunywa pombe
Baadhi wananchi wa mjini kakonko waliokuwa katika
kazi ya kuchimba makaburi manne kwa wakati mmoja wanaeleza maskitiko yao nakusema vitendo hivi vimekuwa vikijirudia marakwamara
watu wengi kupewa sumu hali inayowafanya kuishi kwa hofu katika jamii
Mkuu wa wilaya hiyo, Peter Toyima amewataka wakazi wa
wilaya hiyo kuachana na mambo hayo kuwadhulu watu wasiyokwa na hatia bali kila
mtu anatakiwa kutambua uthamani wa Binadamu mwenzake
Hata hivyo mkuu huyo wawilaya amesema kuwa mtu mmoja
anashikiliwa na jeshi la polisi akithumiwa kuhhusika na mauwaji hao na jeshila
polisi linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha tatizo
Dr Fadhili Seleman mganga mkuu Wilaya kakonko |
Maoni
Chapisha Maoni