Watumia zaidi ya masaa sita kutafuta Maji

Watumia zaidi ya masaa sita kutafuta Maji

Muhingo Mwemezi Mwananchi

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha kigendeka kata ya busagara wilayani kibondo mkoani kigoma wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji hali inayo walazimu kutumia zaidi ya masaa sita wakitafuta huduma ya maji huku wakikwama katika shughuli nyingine za  kimaendeleo.

Wakizungumza na gazeti la mwananchi wakazi ambao ni Jahson Kabuka na Zabron Reuben wamedai kuwa kijiji hicho kina kisima kimoja baada ya visima vinne kuharibika na hata kilichopo kinatoa maji kidogo sana na kwakuwa kijiji kina idadi ya watu 9800 ambapo hupelekea mrundikano wa watu katika kisima hicho na kuzua fujo zisizo kuwa na msingi huku baadhi yao wakitoleana matusi na kugombana hali inayo hatalisha usalama wao.

Nae  mmoja wa wakazi hao bi Helen Kavula .amesema hata hivyo kutokana na mda mwingi wanao tumia katika kutafuta maji,  kumepelekea kuwepo kwa kukwama kwa shughuli za kijamii katika utafutaji wa mahitaji ya kifamilia  na hivyo kuomba serikali kuwasaidia ilikuweza kutimiza adhima ya maisha bola kwa kila mwananchi.

Nae bi. Amesema Hata hivyo  hali hiyo imepelekea kusambalatika kwa baadhi ya ndoa kutokana na wanaume wengine kuwatuhumu wake zao kuwa huenda mda wanaokuwa katika shughuli ya utafutaji maji hujihusisha na tabia nyingine chafu kwani masaa yanayo tumika katika utafutaji wa maji hayo unakuwa mwingi saana.

Hata hivyo baadhi ya walimu walioajiliwa hivi karibuni katika za msingi kumshindwina kigendeka ambao ni Paol Machibta na Jesca Lazaro wamelalamikia hali ngumu  ya upatikanaji wa maji na kuto kidhi mahitaji na hivyo kuwalazimu kutumia mda mwingi kutafuta maji huku wakipoteza mda ambao wangetumia katika kuandaa maandalio ya ufundishaji hali ambayo wameeleza kuwa hupelekea kushuka kwa kiwango cha cha ufundishaji kwa walimu hao.

Aidha wameitaka serikali kulivalia njuga swala hili mapema kwani huweza kusababisha idadi kubwa ya walimu wanaopangiwa katika mazingira hayo kutumia kigezo hicho kwa kuhama shule kwa kuogopa galama za maisha hali ambayo wameeleza kuwa kitaaluma huwaathili wanafunzi na kusababisha kiwango cha taaluma kushuka.

Nae  Mwenyekiti wa  kijiji hicho alisema kuwa tatizo lipo na ili waweze kukabiana nalo wameamua kweka utaratibu kwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi kutoa shilingi miatano kila mwezi ili kuweza kukarabati visima vilivyoharibika.  

Kwa upande wake mtendaji wa kata ya Busagara Bw.Baruani Bwimo amesema hata hivyo tatizo hilo ni la muda mrefu ambapo wanafanya utaratibu wa kushilikisha wananchi kutoa michango yao ilikuweza kupata kisima kingine  na kupungunza adha kwa wakaazi huku akisema baadhi ya wananchi hulazimika kutumia maji ya vijito vidogovidogo ambavyo navyo umbali mrefu na sio salaama kwa afya zao

Pamoja na mambo mengine Baruani amesema kuwa katika kamati ya maendeleo ya kata kuomba msahada  katika mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwa kutengeneza andiko ili waweze kuleta miradi ya maji kwenye vijiji vinavyounda kata hiyo kikiwemo Kigendeka
Mwisho



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao