Mtoto huyu anadaiwa ameibwa, na kutelekezwa kwenye basi la Abiria na hadi sasa hajapata wazazi wake
Katika vintendo vinavyotajwa kuendelea kufanywa na
wafanyakazi wa ndani kwa kuwanyanyasa vimeendele kushika kasi baada ya motto
mwenye umri wa miaka mitatu hadi mine kutelekezwa kwenya basi abiria jijini
Mwanza na mtu anayesadikiwa kuwa mtumishi wa nyumbani kwao.
Mtoto huyo ambaye anaweza kutaja jina lake tu
la Antoni, na wala hawezi kutaja majina
halisi ya wazazi wake bali anataja mzazi wake wa kiume anaitwa Baba
Antoni na mama Antoni, alikutwa amelekezwa kwenye Basi la Abiria la Kampuni ya
Horeza, linalofanya safari zake kutoka Kibondo mkoani kigoma kuelekea jijini
mwanza
Wahudumu wa gari hilo walishangaa kuona abiria wote
wametelemka na kumshangaa mototo huyo amebaki peke yake bila mtu mzima anaye
weza kumsaidia ndipo walipojaribu kuwauliza baadhi ya abiria waliokuwa
wamesalia nje ya gari gabla ya kuelekea majumbani mwao juu ya motto huyo
inadaiwa mwanamume mmoja alijibu kuwa wakati wa safari alikuwa na binti mmoja
anayesadikiwa kuwa na umri wa miaka kumi hivi.
Aidha wakati wa kutelemka kwenye gari walishangaa binti huyo
anatoka peke yake na alipoulizwa mbona
mototo huyu una mwacha alisema kuwa yeye hamjui na kuamua kumuacha peke yake
bila msahada ndipo wahudumu hao waliamua kurudisha kibondo mkoani kigoma ili
kutafuta wazazi wake lakini hawakuweza kupatika na baadae kuamua kumpeleka
kituo cha polisi mjini kibondo.
Kwa mujibu wa maelezo ya polisi wazazi wa motto huyo wazazi
wake hawajapatikana na amechukuliwa na msamaria mwema anayeitwa Josephin Joseph
ambaye ni mfanya kazi wa Jeshi la Polisi hadi hapo wazazi wake watakapopatikana
kwa maana yeye hawezi kujieleza vizuri kulingana na umri wake
Hata hivyo baadhi ya wakazi wa mji wa kibondo
waliokusanyika mumtambua motto huyo, wametoa maoni yao kuwa ni vizuri jamii ikawa makini hasa
pale mtu anapohitaji mfanya kazi wa ndani kuhakikisha anafahamu kwao na wazazi
wake walipo ili kuepuka madhala zaidi
Mtoto Anton anayedaiwa kuibwa na mtu anayesadikiwa ni mfanyakazi wa ndani na kutelekezwa kwenye basi la abiria |
Maoni
Chapisha Maoni