Kakonko yapitisha Rasmu ya bajeti Bilion 26 mwaka 2015/16
Mwemezi Muhingo Mwananchi
Katika mwaka wa fedha wa 2015/16 Halamashauri ya wilaya
kakonko Mkoani imepanga kukusanya na kutumia jula ya Tsh Bilion 26.4kutoka vyanzo mbalimbali
ikiwemo ruzuku ya serikali kuu bilion 25 na mapato ya ndani tsh milion 436
ambapopo mchango wa serikali kuu ni sawana asilimia 98.3 ya bajet ya
Halmashauri
Akisoma taarifa yake wakatati wa kikao cha Baraza la madiwani
kilifanyika mjini kakonko kwa ajili ya
kujadili mipango na Rasimu ya mapendekezo ya Bajeti ya Halmashauri hiyo, kwa
mwaka wa fedha wa 2015/16 Bw, Galpa
Sedoyeka, amesema kuwa vipaumbele vya bajeti hiyo nikujikita zaidi katika
mswala ya elimu
Sedoyeka amesema kuwa
mpango wa mwaka 2015/16 umeandaliwa kwa
kuzingatia vipaumbele na kiutekelezaji
kuboresha utoaji elimu bora ili kuongeza kiwango cha ufaulu kuwaandaa
wanafunzi kuweza kukabiliana na na maisha baada ya kumaliza masomo
Hata hivyo ametaja vipaumbele vingine kujenga Ofisi za
Halmashauri ujenzi wa nyumba za watumishi kwa kushirikiana na Taasisi
mbalimbali kama shilirika la Nyumba la Taifa [NHC] ambalo halmashauri
imeingianalo mkataba wa kujenga nyumba 50
Amesema kuwa mapato ya makusanyo ya ndani yanategemea ushuru
wa masoko ya mipakani mazao na leseni mbalimbali ambapo amedai kuwa wanafanya
utarati kuongeza tozo ili kukabailiana hali halisi kwa kuwa halmashauri hiyo ni
changa imeanzishwa mwaka 2013 na kuanza kufanya kazi mwaka 2014
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nyamtukuza Marko Bajora,
amesema kuwa bajeti hiyo inachangamoto nyingi hasa mapato ni kidogo sana hali
inayoweza kumfanya mwananchi asinufaike kutokana na baeti hiyo kuwa tegemezi
sana asilimia 1.7 ndo mapato ya ndani na
asilimia 93.3 inategemea kutoka serikali kuu hivyo pesa hizo zikichelewa kufika
kwa muda muafaka upo uwezekano halmashauri ikashindwa kujiendesha
Bajeti hiyo kwakuwa inalenga
kumsaidia mwananchi, imepokelewa kwa mawazo tofauti na baadhi ya
wananchi waliohudhulia katika kikao hicho ambapo mmojawao Bw, Mohamed Ismail
ameshauri kuwa lengo la halmashari hiyo nijema ila pale inapotaka kuongeza
ushuru ni vema itengeze miundo mbinu ya kukusanyia tozo hizo kwasababu katika sehemu
kubwa ya wilaya hiyohakuna maeneo maaluma ya kukusanyia mapato kama machinio
hali inayoweza kufanya ukusanyaji kuwa mgumu na kukosa mapato
Mkurugenzi mtendaji waHalmashauri hiyo Bi Zaina Msangi
amesema kuwa pamoja na kuwa bado mambo mengi hayajakaa vizuri wanafanya
mchakato wa kuboresha vyanzo vya mapato ili kuleta mafanikio katika matarajio
yanayokusudiwa
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya kakonko Bw, Juma
Maganga amewataka watendaji wote wa kata na vijiji, kuweza kufanya kufanyakazi kwa bidii uaminifu
katika swala la kukusanya mapato kwakuwa wakati wanawatumia mawakala ni hasara
kubwa iliyopatikana
Pamoja na mambo mengine Maganga amewataka wa nanchi wa
Kakonko kukubali kwenda na mabdiliko ya kimaendeleo yaliyopo kaika nchi yetu
kwa kufuata taratibu na sheria
Aliyasema hayo akiwahasa wananchi kukubali kuwa nampangilio
mzuri wa mji kwa kujenga na kuwa naviwanja vya makazi vilivyopimwa kwa mujibu
wa sheria kufuata miongozo ya Idara ya ardhi.
Aidha alidai kuwa Mji wa kakonko hapo awali ulikuwa ni
kijiji, jamii ilizoea mazingira kutegemeana na wakati uliokuwepo lakini baada
ya serikali kutangaza kuwepo na wilaya na halmashauri katika eneo hilo lazima
watu wakubali kufuata taratibu wanazopewa
Aliwataka kufahamu kuwa idara ya ardhi wilayani hapo, imetoa
elimu kwa kiasi kikubwa kuwa kila aliyekuwa na shamba likapimwa vikapatikana
viwanja zaidi ya vitatu nilazma vinavyobaki itakuwa na mali ya Halmashauri na
mtu aakaye hitaji kuvimili zaidi anatakiwa kulipia kwa mujibu wa taratibu
alikini cha ajabu wengi wao wamekataa kugawana viwanja na Halmashauri hiyo na
kusema kuwa yeyote ambaye hatakubali kufanyahivyo, sheria itachukua nafasi yake
kwa kuchukua na wakuwamilikisha wengine
kama utaratibu unavyosema na kudai kuwa agizo hilo siyo la mtu binafsi bali ni
nchi nzima
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni