Mtendaji wa kata akataliwa, wakijiji afukuzwa kazi katika mkutano wa hadhara
Mtendaji wa kata akataliwa, wakijiji afukuzwa kazi katika mkutano wa hadhara
Wananchi
wa Kijiji cha kigendeka Kata ya Busagara wilayani kibondo mkoa wa kigoma wamemmfukuza
kazi Mtendaji wa kijiji, kukataa kufanyakazi na mtendaji wa Kata kwenye mkutano
mkuu uliofanyika kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo, kwa madai kuwa wote wawili walishirikiana
kugushi mhuri wa ofisi ya kijiji na kugawa ardhi hekali 100 kinyume cha
taratibu
Uamuzi
wa wakazi hao umefikiwa baada kikako
cha uongozi wa kijiji hicho kilichokaa
Tarehe 15.1.2015 baada ya kubaini matatizo hayo, na kumuita mtendaji huyo na
kumueleza makosa yake hali iliyowafanya
wajumbe wa kikao hicho kutokuwa na Imani nae na kumtaka aachie ngazi hatua
iliyofikia mwenyekiti Bw, Yotham Kitwe kuitisha mkutano mkuu wa kijiji ili kutoa
maamuzi.
Awali
mkutanoni hapo, ilidaiwa kuwa mwaka jana tar 24.4.2014 Bw Abeli Fransisco akiwa
ni mwenyekiti wa kitongoji, aliiba mhuri wa Afisa mtendaji wa kijiji na kumgawia Bw, Samsoni Kitwe ardhi ya kijiji hicho ambayo ilitengwa kwa
kulishia mifugo ya jamii ya kijiji hicho na kumshirikisha Afisa
mtendaji wa Kata ya Busagara Bw, Baruani Gwimo nayeye kuchukua uamuzi wa kusaini
barua ya kugawa eneo hilo, Tar 27.4.2014, huku wakijua kuwa ni kinyume cha
taratibu ilitengwa kwa kazi maalumu na
haikutakiwa kumilikishwa kwa mtu yeyote
Baadhi
ya wananchi walitaka Bw, Abel Fransisco
aweze kusamehewa kosa lake
hatua ambayo ilikataliwa
na wengi wakidai kuwa vitendo hivyo vimekithili hapa nchini na kuwafanya
wananchi kukata tamaa na hawakotayari kuharibu kijiji chao kwa sababu ya mtu
mmoja
Fransisco,
anayetuhumiwa kugawa neo hilo ambalo linatwa
kuwa ni zaidi heka 100 amesema kuwa yeye alitoa hati hiyo kwa Samsan Kitwe , kwasababu hakuwa na
mtu wa kumshirikisha maana wakati huo serikali ya kijiji ilikuwa imeshavunjwa
kufuatia uchaguzi wa serikali za mitaa na ofini hapo kulikuwa na maombi hayo
akaona ayafanyie kazi
Kwa
upande wake mtendaji wa kata ya Busagara Baruani Gwimo katika kujitetea kwake
amesema kuwa yeye hakushiriki kuuza eneo hilo
na wala halija uzwa bali samsoni aliomba kuwa anachungia mifugo yake, ila
kilichopo ni uonevu
Anayedaiwa
kugawiwa eneo hilo
bila utaratibu, Bw, Samsoni Kitwe hakuweza kupatikana na kwenye mkutano huo
hakuwepo kwa madai kuwa alipata dahrula iliyomlazimu kusafiri
Hata
hivyo wananchi walimtaka akubali makosa yake ili hata siku nyingine aweze
kujirekebisha na kama Bw, Kitwe aliomba kuchunga
mifugo yake na hati ya kumiliki eneo hilo
alipewa yanini?
Kulingana
na halivyo, Diwani wa kata hiyo, Godwini Sibanilo alimuagiza mtendaji wa
kijijji cha kigendeka kukabidhi ofisi kwa mtendaji wa kata kwakuwa kanuni zina
sema hivyo hadi utaratibu wa kupata mtu atakae chukua nafas yake
Halmashauri
ya kijiji haina uwezo wa kumuwajibisha mtendaji wa kata bali waliamua
kumuandikia mwajili wake amabaye ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya kwa kueleza makosa ya mfanyaka zi wake na
kuwa hawako tayari kufanya kazi nae
Mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya kibondo Bw Judathadius Mboya alipofuatwa kuzunguzia
swala hilo
alikisema yeye ana majukumu ya kazi maalumu hivyo hana muda kwasasa
Maoni
Chapisha Maoni