Wahitimu jkt muwe mabalozi wema kwenye jamii
Mkuu wa mkoa wa kigoma kanali
mstaafu isay machibiya amewataka vijana wanao hitimu mafunzo ya jkt kuwa na
nidhamu katika jamii na kujiepusha na utumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na
zinaa ilikuendelea kuimalisha afya zao.
Kauli hiyo ameitoa wakati
akifunga mafunzo ya kijeshi operation miaka 50 ya muungano mujibu wa sheria
kundi la pili katika kikosi cha jeshi 824 kj kilichopo Kanembwa wilayani
kakonko mkoani kigoma
Bw.Machibiya amesema idadi
kubwa ya vijana imekuwa ikijihusisha
katika matukio mawili hatalishi ikiwa ni pamoja na utumiaji wa madawa ya
kulevya pamoja na zinaa ambavyo vimemaliza vijana wengi wakiwa nguvu kazi ya
taifa.
Nao vijana waliohitimu
mafunzo hayo ya awali kwa mujibu wa sheria wakiapa mbele ya mkuu wa mkoa na viongozi
mbalimbali sambamba na wananchi wameahidi kulitumikia taifa kutokana na mafunzo
waliyo pata ilikuhakikisha nchi inaenderea kuwa ya amani upendo na utulivu
Katika Liasra yao vijana hao waliokuwa wakihitimu mafunzo hayo
iliyosomwa na Happynes wilison, walieleza changamoto zinazowabili kikosini
ikiwa ni ukosefu wa gari la kubeba wagonjwa hali inasababisha usumbu mara
wanapopatikana wagonjwa ikilinganishwa na idadi watu waliopo kwenye eneo hilo .
Aidha waliiomba serikali
kuongeza muda wa mafunzo uongezwe iwe miezi sita badala ya miezi mitatu
inayotumika sasa ili kuwaweka vijana katika hali nzuri zaidi katika kulitumikia
Taifa.
Hata hivyo mkuu wa kikosi
hicho cha 824 kj kanembwa jkt Luten Kanal Castory Bwegoge amesema kuwa vijana
walioanza ni vijana 1333 waliomaliza
mafunzo elf 1 miamoja 27 wavulana wakiwa mia 7 stini na2 na wasichamia3 stini
65 wengine 206 walishindwa kumaliza kwasababu mbalimbali ikiwa vifo na matatizo
ya kiafya, ambapo wengi wa wahitimu hao ni
walimu wa stashahada, cheti, waliomaliza kidato cha sita
Aidha Bwegoge ameleza kuwa
pamoja na changamoto zilizopo, lakini vijana wamejifunza mambo mbalimbali ikiwa
ni kushiriki katika shuguli za kijamii
kazi za ujenzi wa taifa kama kushiriki
katika ujenzi wa majengo ya maabara katika shule za sekondari wilayani
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni