Zitambueni kaya maskini Kwa uaminifu

 Mwemezi Muhingo Mwananchi
 
Meneja uhawishaji fedha kupitia mfuko wa jamii (TASAF)kutoka makao makuu  Bw.Omary malilwa ambaye alimwakilisha mkurugenzi mkuu Tasaf amewataka viongozi watakao pewa nafasi ya kufatilia kaya maskini katika wilaya ya kakonko mkoani kigoma  kuorodhesha kaya hizo bila kuwepo ubaguzi na kuwa waaminifu katika kazi hiyo.

Kauli hiyo allitoa jana wakati wa kikao kilicho wakutanisha madiwani na viongozi mbalimbali wa serikali  ikiwa ni kwa awamu ya tatu kufanyika wilayani humu kwa lengo la  kunusuru kaya maskini katika nyanja mablimbali ikiwa ni pamoja na elimu,afya,hususa kwa wale ambao hawana uwezo wa kumudu ghalama hizo.

Bw.Malilwa amesema mara nyingi fulsa kama hizi zinapo anzishwa huingiliwa na wanasiasa kwa kutaka kujipatia umarufu na kuvuruga mpango uliokusudiwa na serikali  na hivyo amewataka wanansiasa kutotumia nafasi hiyo kwani mfuko wa jamii haubagui chama,kabila au dini ya mtu.

 Jumla ya kaya 920,000 kwa nchi nzima sawa na asilimia 14 zinazo ishi katika mazingira magumu  zinatarajia kunufaika kutoka katika mfuko wa jamii ‘tasaf’ na kwamba mpango huu ni endelevu hasa kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano

 Ambapo mkurugenzi wa halimashauli ya wilaya ya kakonko Bi.Zaina msangi ameahidi kuwachukulia hatua Viongozi ambao hawatasimamia swala hili kikamilifu.

Wananchi waliohudhulia kikao hicho waliuomba ungozi wa Tasaf kuwa makini katika kuwfanya utambuzi wa walengwa ambao ni watu waoishi katika mazingira magumu kwani juhudi hizi zinaweza  zisifanikiwe kwani mara nyingi kumekuwa kukitoke vitendo visivyoridhishwa kwa le wanaopewa dahamana kama hizo ha upande wa vijiji kwa miradi mbalimbali

Mmoja wana wananchi hao Bi Husna Rajabu alisema kuwa kuna hatari ya mpango huo wa kusuru kaya masikini kufikia malengo kama uongozi hauta kuwa na utaratibu kujiridhika kama taarifa za walengwa ni sahihi au ni vinginevyo

Bi husina alisema kuwa mara nyingi kumekuwepo na tabia kwa watendaji kuatazama watu wanaotoka katika famili zenye uwezo na kuwaacha wale wano kusudiwa hasa katika maswala ya elimu na mengineyo

Hata hivyo maliwa alijibu kuwa hali hiyo hawatarajii kutokea kwani watakao fanya utambuzi ni mkutano mkuu wa kijiji katika maeneo husika maana wanavijijindiyo wanaowafahamu wenzao waliokatika mazingira magumu nabaade wakiorodheshwa, mkutano mwingine utaitishwa kwa ajili ya kuhakiki kama kilichofanyika mwanzo ni sahihina wananchi ndiyo watakaofanya kazi hiyo kwa kushirikiana na wawezeshaji

Adha maliwa ameewataka wanasiasa kuacha kuingilia mpango huo kwani hapo kisiasa bali ni kutoa huduma kwa wananchi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji