Dc awataka Viongozi wote serikali za mitaa waliochaguliwa hivi karibuni kutimiza wajibu wao kila mmoja na kuondoa tofauti za vyama
Kibondo; Mkuu wa wilaya ya Kibondo mkoani kigoma bw.
Venance Mwamoto amewata viongozi waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za
mitaa uliofanyika mapema mwaka jana kufanya kazi kwa bidii katika kuchochea
maendeleo ya wilaya.
Kauli hiyo aliitoa wakati
akizungumza na viongozi hao katika Tarafa ya mabamba kata ya mabamba mara baada
ya kuapa kulitumikia taifa na wananci kwa moyo mmoja na ushilikiano katika
kudhibiti matukio machafu.
Bw.mwamoto amesema katika
utawala wa serikali ngazi ya chini ni kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa na
hivyo wao wanapaswa kluwa chachu ya kuchochea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa juu ya uharifu.
Mwamoto alisema kuwa uongozi
ngazi ya vitongoji ni hatua muhimu sana
kwani hakuna serikali kuu bila kuanzia ngazi ya kitongoji hivyo ni vyema
viongozi hao wajiamini na kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana ili
kufikia mafanikio.
Aidha aliwataka kuachana
tabia ya mashindano ya kisiasa ambayo
kwa sasa hayawezi kuleta tija ila lililopo ni kushirikiana watu wa vyama vyote
kwani wote wanajenga nchi moja. Kinachotakiwa ni uadilifu katika utendaji wa
kazi
Nao baadhi ya viongozi hao
waliochaguliwa hivi karibuni ambao ni Samweli Jonasi na Halima Abdalah katika uchaguzi wa serikali za mitaa wameahidi
kuwatumikia wananchi waliowapa dhamana hiyo ya kuwa madarakani kwa ushilikiano
bila kujali itikadi za vyama
Maoni
Chapisha Maoni