Wampinga Kabila kuwania urais nchini DRC
Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamewafyatulia risasi waandamanaji kwenye mji mkuu Kinshasa walio na hasira katika kile kinachoonekana kama jitihada za kutaka kuongoza uongozi wa rais Joseph Kabila.
Watu kadha walitolewa eneo la kati kati mwa mji wakiwa na majeraha ya risasi ambapo pia kulitoka makabiliano kwenye chuo kikuu cha mji huo.
Milio ya risasi iliripotiwa katika maandamano mengine katika mji ulio mashariki wa Goma.
Watu kadhaa walipatikana na majeruhi ya risasi katikati mwa mji huo huku ghasia zengine zikiripotiwa katika katika chuo kimoja kikuu.Viongozi wa upinzani waliitisha maandamano hayo baada ya bunge dogo kuidhinisha sheria siku ya jumamosi inayoagiza kufanyika kwa hesabu ya idadi ya watu kabla ya uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka ujao.
Wabunge hao wa upinzani wamesema kuwa mpango huo utachelewesha uchaguzi huo ambao umekuwa ukingojwa kwa hamu kwa miaka kadhaa.
Rais Joseph Kabila ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 15 amehudumu miula miwili na hawezi kuwania tena urais kulingana na katiba.
rais wa Drc Congo Joseph Kabila |
maandamano Drc Congo |
Bunge kuu linatarajiwa kuungazia mswada huo wa uchaguzi hii leo.
Maoni
Chapisha Maoni