Machapisho

Mahakamani kwa kujifanya Afisa wa usalama wa Taifa

Mahakamani kwa kujifanya Afisa wa usalama wa Taifa Mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es salaam amehukumiwa kifungo cha miezi 24 jela au faini ya shilingi laki moja na nusu katika mahakama ya wilaya ya kibondo mkoa wa kigoma, baada ya kukili makaosa ya kujifanya mtumishi wa serikali wa jeshi la wananchi Tanzania na kujifanya afisa usalama wa taifa   Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya kibondo bw Erick Marley mwendesha mashitaka wa polisi bw Frank Ruvanda amemtaja mtu huyo kuwa ni Wiston Ezekiel Bulinjie mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa kinyerezi dar es salaam Bw Ruvanda amesema kuwa mnamo Agost 12 mwaka huu majira ya saa 9 alasiri bw Bulinjie alikwenda kikosi cha 824 KJ kanembwa Jkt wilayani kakonko alijitambulisha kwa Erast Sebasitian Tesha kuwa yeye ni askari wa jeshi la wananchi Tanzania kitu ambacho hakikuwa cha kweli , tarehe hiyo hiyo majira ya saa11 jioni akiwa kibondo mjini alijitambulisha kwa Godifrey Mpigwa kuwa yeye ni afisa usalama wa taifa K...

Mahakamani kwa kusababisha kifo kwa kumpa muwa unaosadikiwa kuwa na sumu

Mahakamani kwa kusababisha kifo kwa kumpa muwa unaosadikiwa kuwa na sumu Mkazi wa kijiji cha kumsenga wilayani kibondo mkoani kigoma amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya kibondo kwa tuhuma za mauaji ambapo inasadikika kuwa alimpa muwa wenye sumu bw Matane Ndegea na kusababisha kifo chake Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya kibondo bw Mulokozi Kamuntu mwendesha mashitaka wa polisi bw Frank Ruvanda amemtaja mtu huyo kuwa ni Sintegeza Ally mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa kijiji cha kumsenga Bw Ruvanda amesema kuwa mnamo September 08 mwaka huu majira ya saa tisa alasiri bw Sintegeza ally  kwa makusudi alimuua  bw Matane Ndegea kwa kumpa muwa wenye sumu ambao ulipelekea kifo chake Hakimu mkazi bw Kamuntu ameahilisha kesi hiyo mpaka itakapotajwa tena September 30 mwaka huu na mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauji hivyo mshitakiwa yuko rumande kutokana na kwamba kesi yake haina mdhamana ...

SERIKALI KUVIHAKIKI VYAMA VYA KIJAMII

SERIKALI imedhamiria kuanza mchakato wa kuhakiki vyama vya kijamii ili kuboresha huduma zinazotolewa na vyama hivyo nchini tangu kuanzishwa kwake. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Isack Nantanga, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari. Alisema uhakiki huo utaanza rasmi Oktoba mwaka huu ambapo vyama visivyo na sifa ya kuendelea kuwa katika Daftari la Msajili vya Vyama vya Kijamii, vitafutwa kabisa. Akizungumzia sababu zinazoweza kusababisha vyama hivyo kufutwa katika daftari hilo, alisema ni pamoja na kutolipa ada za mwaka kwa wakati na kutowasilisha kwa Msajili taarifa za kila mwaka za utendaji kazi wa chama. Sababu nyingine ni chama kufanya shughuli tofauti na zile ambazo ziliandikishwa kwenye katiba ya chama husika. "Ili kuvishirikisha vyama husika, kabla ya kuanza uhakiki huu Wizara itachapisha katika baadhi ya magazeti majina ya vyama vyote vya kijamii vilivyopo katika kumbukumbu za daftari hilo. "Baa...

TANZANIA YASHAURIWA KUWEKEZA KATIKA MAENDELEO YA WATU WAKE

T ANZANIA inatakiwa kuwekeza zaidi katika watu wake ili kuweza kufikia maendeleo ya kweli na endelevu. Imesemekana, kuwekeza katika watu kumethibitisha kuwa moja ya sababu kubwa ya kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya mataifa mbalimbali na pia kuwa kati ya mambo muhimu yanayozingatiwa na wawekezaji wanapochagua maeneo ya kuwekeza. Kauli hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Jamii na Uchumi (ESRF), Dkt. Hoseana Lunogelo, alipokuwa akiongea wakati wa mkutano watatu wa kitaifa wa taasisi hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. "Kwa kuwekeza katika watu, Serikali itahakikisha kuwa wananchi wanawezeshwa kuendesha maisha na kuwa wenye mchango kwa jamii," alisema Dkt.Lunogelo. Alisema kuwa kuwepo kwa nguvukazi kubwa yenye ujuzi ni faida kwa wawekezaji wa ndani na nje. Alisema kuwezeshwa huko kunaleta ujuzi, maarifa na ufanisi ambao huimarisha ubora wa nguvukazi. "Nguvukazi yenye ujuzi ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa rasi...

Mwanafunzi wa Darasa la tatu abakwa,

Mwanafunzi wa Darasa la tatu abakwa, Mwanafunzi wa Darasa la tatu katika shule ya Msingi Busunzu B Wilayani Kibondo amelazwa katika hospitali ya Wilaya  hiyo  baada ya kubakwa  na kijana mmoja alietajwa kwa jina la Lukelegwa Maneno Mkazi wa Kijiji cha Busunzu B. Akizungumza na na waandishi wa habari , Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Dr. Adam Jonathani amesema mtoto huyo wa Kike mwenye umri wa Miaka 10, amepata majeraha makubwa  na inaonyesha amechomwa na kitu chenye ncha kali sehemu zake za sili baada ya kubakwa. Dr. Jonathani amesema mtoto huyo hali yake inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu hospitalini hapo na kwamba kwa sasa wanaendelea kumtibu  Ugonjwa wa Maralia uliongundulika katika hatua za uchunguzi wa awali. Hata hivyo Dactari huyo hakuwa tayari kuzungumza  kwa uwazi juu ya hali halisi ilivyo kulingana na uchunguzi ulifanywa na waganga wa hospitali hiyo juu ya huyo mtoto. Aidha...

Ukawa wasumbua vichwa vya Baadhi ya Wabunge Dodoma

Picha
KATIKA hali inayoonekana kama kutaabishwa na wajumbe wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Swmweli Sita Samuel Sitta, jana aliamua kueleza hali halisi ilivyo kwa takribani dakika sita akiwa ndani ya ukumbi wa Bunge wakati mjadala wa katiba ukiendelea  na kuwaita  wajumbe kuwa  ni waigizaji. Hatua hiyo ya Sitta, ilibadili upepo wa Bunge kwa muda, kwani baadhi ya wachangiaji wa mjadala wa sura za rasimu ya katiba, nao waliamua kuanza kujadili hoja na kujikita kuwataka wana  UKAWA kuwa wakeli. Miongoni mwa wajumbe waliochepuka kwenye mjadala na kuwajadili UKAWA ni Mwenyekiti wa UPDP, Fahami Dovutwa, ambaye alizungumzia kuhusu makubaliano ya kikao baina ya vyama vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), na Rais Jakaya Kikwete. Licha ya kuwafurahisha wajumbe wa CCM, Dovutwa alijikuta akitofautiana na Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo (UDP), pale alipokiri kwamba yeye, Cheyo na A...