Machapisho

Kibondo;Wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi wameeleza kukabiliwa na tatizo la walimu wanaopata ajira za muda katika shule zao na kisha kuondoka baada ya muda mfupi, kuwa hali hiyo inawahathiri kimasomo na kupelekea kushuka kwa kiwango cha elimu katika shule hizo tofauti na mategemeo yao

Picha
Lidia  ladislaus Mwanafunzi shule ya sekondari Bishop Mpango Baadhi ya wanafunzi shule ya sekondari Mt Thomas More Kibogora Jeremia Gwegenyeza makamu mwenyekiti  CHAMA CHA WAMILIKI WA SHULE BINFSI  WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI bISHOP mPANGO  Kibondo; Wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi wameeleza  kukabiliwa na tatizo la walimu wanaopata ajira za muda katika shule zao na kisha kuondoka baada ya muda mfupi, kuwa hali hiyo inawahathiri kimasomo na kupelekea kushuka kwa kiwango cha elimu katika shule hizo tofauti na mategemeo yao Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanafunzi hao, ambao ni Peter Lyoba kutoka shule ya sekondari Kibogora iliyoko wilayani Kakonko, na Lidia Shija shule ya Sekondari Bishop Mpango ya wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wamesema  kwakuwa kila mwalimu ana namna yake ufundishaji , hivyo wanapobadirishiwa walimu kila mara uwasababishia usumbufu kuanza upya kumuelewa ‘’Wakuu wengi...

Kakonko;Naibu waziri Ofisi ya Rais serikali za mitaa Tawala za mikoa Tamisemi Seleman Jafo amewataka wakuu wa Idara za halmashauri za wilaya kuhakikisha wanashirikiana na wafanyakazi walio chini yao katika utendaji kazi ili kuleta tija na kuondoa kukata tamaa kwa wafanyakazi

Kakonko; Naibu waziri Ofisi ya Rais serikali za mitaa Tawala za mikoa Tamisemi Seleman Jafo amewataka wakuu wa Idara za halmashauri za wilaya kuhakikisha wanashirikiana na wafanyakazi walio chini yao katika utendaji kazi  ili kuleta tija na  kuondoa kukata  tamaa kwa wafanyakazi Wito huo aliutoa jana  alipokuwa akizungumza na Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma katika ziara yake ya kutembelea baadhi ya mikoa na wilaya kukagua shuguli za maendeleo Jafo alisema kumekuwepo na baadhi ya wakuu wa idara ambao hawana mausiano mazuri na wafanyakazi wa nchini yao hali inayopelekea wengi kukata tamaa ya kazi na kufanya shuguli za maendeleo ya kuwahudumia wananchi kutokuwa na mafanikio ‘’Kitu cha kusikitisha ni pale mfanyakazi anapoka muda mrefu bila kupandaraja huku wanaojiriwa nyuma yake wanapanda kisa hajatoa rushwa na rushwa mbaya zilizopo ni rushwa za ngono jamani wakuu wa idara watendeeni watu mema maafisa utumishi jipangeni vizuri kwa...

Marekani na Urusi zimelaumiana vikali kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mashambulizi dhidi ya msafara wa misaada nchini Syria, pamoja na hatua ya kuvunja mkataba wa kusitisha mapigano.

Picha
Moja ya malori yaliyoteketezwa Marekani na Urusi zimelaumiana vikali kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mashambulizi dhidi ya msafara wa misaada nchini Syria, pamoja na hatua ya kuvunja mkataba wa kusitisha mapigano. Wamarekani wamekuwa wakiamini kuwa Urusi ndio iliyoshambulia msafara huo, huku Warusi wakilipinga hilo. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi John Kerry, alitoka nje ya lugha ya kidiplomasia kwa kutumia dhihaka zaidi. Huku mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov akipinga hisia hizo kali kwa kuorodhesha mifano kadhaa kutetea nchi yake. Aidha ametaka pia kufanyika Licha ya majibizano makali, Urusi na Marekani zilikubaliana kwa pamoja kuongoza mkutano wa mataifa 23, yanayoiunga mkono Syria ambao utafanyika mjini New York, baadaye leo. Katika hatua nyingine Umoja wa Mataifa umesema unajiandaa kuanza tena kutoa misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyozingirwa nchini Syria, baada ya kusitishwa kwa usambazaji wa misaada kufuatia shambulio hilo. Mjumbe ...

Maafisa wa jeshi la ulinzi wa rais wamehusika katika shambulio dhidi ya makao makuu ya chama cha upinzani, watu wawili waliojeruhiwa wameambia BBC.

Picha
Add caption Maafisa wa jeshi la ulinzi wa rais wamehusika katika shambulio dhidi ya makao makuu ya chama cha upinzani, watu wawili waliojeruhiwa wameambia BBC. Makao makuu ya vyama vitatu vya upinzani katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo yaliteketezwa moto katika mashambulio ya usiku kwenye mji mkuu Kinshasa. Kumekuwa na miili ya watu wawili ilioteketezwa moto katika ofisi hizo zilizoharibiwa za muungano mkuu wa upinzani DRC (UDPS). Msemaji wa jeshi la Congo ameiambia BBC hana la kusema kuhusu shutuma hizo. Upinzani unasema zaidi ya watu 50 wameuawa Jumatatu wakati wa maandamano kumpinga rais Joseph Kabila. Serikali inasema idadi ya waliouawa ni watu 17. Vikosi vya usalama vimeshutumiwa kwa kutumia risasi dhidi ya waandamanaj hao wa amani waliotaka kutolewa tarehe ya uchaguzi wa urais nchini.

Kakonko; Watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kulinda mali za umma huku wakitambua kuwa ni kodi za na ni kwa manufaa yao wenyewe hivyo hawana budi kutoa taarifa katika mamlaka husika pale wanapoona kuna dalili za kuhodhiwa au kuhujumiwa kwa mali hizo

Picha
Baadhi ya wananchi na wafanyakazi wa halmashauri ta kakonko waliohudhiria utilianaji wa sahihi mkataba ujenzi wa halmashauri hiyo kati yake na kampuni Magaco ya mjini Dodoma Kakonko; Watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kulinda mali za umma huku wakitambua kuwa  ni kodi za na ni kwa manufaa yao wenyewe hivyo hawana budi kutoa taarifa katika mamlaka husika pale wanapoona kuna dalili za kuhodhiwa au kuhujumiwa kwa mali hizo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Lusubiro Joel akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya wilaya hiyo na Mkandarasi Magacon Constraction limited ya Mjini Dodoma juzi, Lusubiro alisema watu wengi ubaki wakilalamika  badala ya kutoa taarifa ili kuzuia uharibifu zaidi huku akiwasisitiza wananchi kutembelea eneo la ujenzi wa osifi hizo na kuhoji pale wasipoelewa mambo juu ya mambo yanayoendelea ‘’Tumeamua katika halmashauri yetu kufanya mambo wazi hale yale ...

Madereva nane wa malori kutoka nchini Tanzania na wengine wanne kutoka Kenya wameokolewa baada ya kushikwa mateka mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo

Picha
Madereva nane wa malori kutoka nchini Tanzania na wengine wanne kutoka Kenya wameokolewa baada ya kushikwa mateka mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo. Madereva hao walitekwa nyara katika mkoa ulio kusini wa Kivu siku ya Jumatano. Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Tanzania ilisema kuwa watekaji nyara wao walikuwa wakiitisha fidia ya dola 4,000 kwa kila dereva. Hata hivyo waziri wa masuala ya ndani nchini Congo Zakwani Salehe, alisema kuwa hakuna fidia iliyolipwa na ni wanajeshi waliowaokoa madereva hao Aliwataja watekaji hao kama majambazi na haijabainika ikiwa walikuwa na uhusiano na kundi lolote la waasi linaloendesha shughuli zake mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo. Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Bukavu anasema kuwa visa vya utekaji nyara kwa fidia vinazidi kuongezeka Malori hayo yalichomwa moto na madereva wake kutekwa nyara Mara nyingi bidhaa husafirishwa kwende DRC kutoka mataifa jirani kwa njia ya barabara

Umoja wa Mataifa unasema kuwa idadi ya watu waliokimbia nchi ya Sudan Kusini kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo imepita watu milioni moja

Picha
Umoja wa Mataifa unasema kuwa idadi ya watu waliokimbia nchi ya Sudan Kusini kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo imepita watu milioni moja. Idadi hiyo inajumuisha zaidi ya watu 185,000 ambao wameikimbia nchi kufuatia mapigano mapya yaliyoanza mwezi Julai. Zaidi ya watu milioni 1.6 nao wamelazimika kuhama makwao ndani ya Sudan Kusini. Kati ya hao wakimbizi 373,626 wameingia nchini Uganga huku theluthi moja kati yao wakiwasili tangu mwezi Julai na 20,000 wiki iliyopita. Wale wanaowasili sasa wanasema kuwa kuna mapigano mapya huku raia wakishambuliwa na makundi yaliyojihami ambayo hupora, huwadhulumu kimapenzi wanawake na wasichana na kuwaingiza jeshini vijana wa kiume. Wakimbizi 292,000 waliingia nchini Ethiopia huku 11,000 wakivuka na kungia Gambella wiki iliyopita. Wale wanaowsili kwa sasa wanatoka jamii ya Nuer wakiwemo watoto 500 wasioandana na wazazi. 247,317 wamewasili nchini Sudan, 1800 wakiwasili kila mwezi katika jimbo la White Nile na mafuriko yakiwa...