Machapisho

Steven Gerrard kuihama Liverpool

Picha
Nahodha wa timu ya Liverpool ya Uingereza Steven Gerrard ataondoka katika klabu hiyo wakati mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. Gerrard, mwenye umri wa 34, alikuwa huru kusaini makataba wa awali na timu ya nje siku ya Alhamisi na anaaminika kutatakiwa na vilabu vya Marekani. Gerrard, ambaye alianza kuichezea Liverpool mwaka1998, hatahamia katika klabu nyingine ya Uingereza. Liverpool ilimpa Gerrard mkataba mpya mwezi Novemba na atatoa taarifa kuhusu mustakhabali wa maisha yake ya soka Ijumaa. Rais wa klabu ya LA Galaxy ya Marekani Chris Klein amekataa kusema lolote kuhusu klabu yake kumsajili Gerrard, ambaye alifunga penalti mbili katika matokeo ya sare ya 2-2 na timu ya Leicester City katika mechi iliyochezwa siku ya Mwaka Mpya 2015.

Mshukiwa wa mauaji Kenya na TZ afariki

Picha
Mmoja wa watu waliopanga mashambuliz ya kigaidi kwenye balozi za marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 ameaga dunia kabla ya kufikishwa kizimbani mjini New York. Wakili wa Abu Anas al-Liby amesema kuwa afya ya mshukiwa huyo ilizorota kwa haraka na inakisiwa aliaga dunia kutokana na maradhi ya saratani ya ini. Bwana al-Liby alikamatwa na vikosi maalum vya marekani nchini libya mwaka 2013. Alilalamika kuwa alikuwa ametekwa na kudhalilishwa Amekana kuhusika kwenye mashambulizi ya Nairobi na Dar-es- salam ambapo zaid ya watu 220,000 waliuawa.

Mtoto huyu anadaiwa ameibwa, na kutelekezwa kwenye basi la Abiria na hadi sasa hajapata wazazi wake

Picha
Katika vintendo vinavyotajwa kuendelea kufanywa na wafanyakazi wa ndani kwa kuwanyanyasa vimeendele kushika kasi baada ya motto mwenye umri wa miaka mitatu hadi mine kutelekezwa kwenya basi abiria jijini Mwanza na mtu anayesadikiwa kuwa mtumishi wa nyumbani kwao. Mtoto huyo ambaye anaweza kutaja jina lake tu la Antoni, na wala hawezi kutaja majina   halisi ya wazazi wake bali anataja mzazi wake wa kiume anaitwa Baba Antoni na mama Antoni, alikutwa amelekezwa kwenye Basi la Abiria la Kampuni ya Horeza, linalofanya safari zake kutoka Kibondo mkoani kigoma kuelekea jijini mwanza    Wahudumu wa gari hilo walishangaa kuona abiria wote wametelemka na kumshangaa mototo huyo amebaki peke yake bila mtu mzima anaye weza kumsaidia ndipo walipojaribu kuwauliza baadhi ya abiria waliokuwa wamesalia nje ya gari gabla ya kuelekea majumbani mwao juu ya motto huyo inadaiwa mwanamume mmoja alijibu kuwa wakati wa safari alikuwa na binti mmoja anayesadikiwa kuwa na umri wa miaka k...

Timu ya Nyarugusu juu

Michezo  Mwemezi Muhingo Nyarugusu fc yaivunda Kasana fc mikwaju ya mabao 4 kwa 0 wakati wa kusherekea mwaka mpya 2015 mechi iliyochezwa katika uwanja wa mpira wa miguu kata ya mabamba wilayani kibondo mkoani kigoma. Akizungumza na gazeti la mwananchi Msimamizi wa ligi ya mwaka mpya Bw.Jamal Abdala Tamimu aliesema wameamua kuanzisha ligi ya mwaka mpya kwa lengo la kuwakutanisha vijana wa kata ya mabamba na wananchi ilkikusherekea mweaka mpya 2015 Aidha    Bw.Tamimu amesema michezo ikiwa ni ajila binafsi kwa vijana ameamua kuanzisha mashindano ya mara kwa mara ilikuwaweka vizuri vijana kisoka na kuwaepusha kutumia mda mwingi wakiwa katika magenge na mijadala ambayo haina tija ya maendeleo kwao. Katika kusherekea sikuu ya mwaka mpya kumechezwa michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na riadha,mpira wa pete,voribal,mpira wa miguu,na michezo mingine yote ikiwa na rengo la kudumisha michezo na kuwawerka wananachi pamoja. Hapo Jan1 timu ya nyaruugusu fc ilishuka...

Wahitimu jkt muwe mabalozi wema kwenye jamii

Picha
Wahitimu jkt muwe mabalozi wema kwenye jamii Issa Machibya Rc Kigoma Mkuu wa mkoa wa kigoma kanali mstaafu isay machibiya amewataka vijana wanao hitimu mafunzo ya jkt kuwa na nidhamu katika jamii na kujiepusha na utumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na zinaa ilikuendelea kuimalisha afya zao. Kauli hiyo ameitoa wakati akifunga mafunzo ya kijeshi operation miaka 50 ya muungano mujibu wa sheria kundi la pili katika kikosi cha jeshi 824 kj kilichopo Kanembwa wilayani kakonko mkoani kigoma Bw.Machibiya amesema idadi kubwa ya vijana imekuwa ikijihusisha  katika matukio mawili hatalishi ikiwa ni pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na zinaa ambavyo vimemaliza vijana wengi wakiwa nguvu kazi ya taifa. Nao vijana waliohitimu mafunzo hayo ya awali kwa mujibu wa sheria  wakiapa mbele ya mkuu wa mkoa na viongozi mbalimbali sambamba na wananchi wameahidi kulitumikia taifa kutokana na mafunzo waliyo pata ilikuhakikisha nchi inaenderea kuwa ya amani u...

Katibu Mkuu Kiongozi,amemsimamisha kazi

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda , Eliakim Maswi, Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete. Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia , Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)”ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu. Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim...

Wapiga kura wahofia Ebola Liberia

Picha
Idadi ndogo ya wapiga kura imeripotiwa kwenye kura ya kuwachagua maseneta nchini Liberia. Kura hiyo ilikuwa imeahirishwa mara mbili kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola na huenda hofu ya ugojwa huo iliosababisha watu kukosa kufika kwa vituo vya kupigia kura. Wapiga kura walishauriwa kusimama umbali wa mita moja kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine walipokuwa wakipanga milolongo kupiga kura baada ya viwango vyao vya joto kuchukuliwa na maafisa wa afya. Kwenye taifa jirani la Guinea waandamanaji waliwazuia wafanyikazi wa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF kuweka kituo cha ebola kusini mwa nchi hiyo. Polisi wanasema kuwa mahema yalichomwa na wafanyikazi wakafukuzwa na megenge ya vijana. Uchaguzi wa kuwachagua maseneta nchini Liberia Jamii kwenye sehemu zingine za magharibi mwa afrika zilipinga jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo zikihofia kuwa huenda zikapata maambukizi kutoka kwa wafanyikazi wa kutoa huduma za afya. Uchaguzi wafanyika nchini liberia licha ...