Wapiga kura wahofia Ebola Liberia

Idadi ndogo ya wapiga kura imeripotiwa kwenye kura ya kuwachagua maseneta nchini Liberia.
Kura hiyo ilikuwa imeahirishwa mara mbili kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola na huenda hofu ya ugojwa huo iliosababisha watu kukosa kufika kwa vituo vya kupigia kura.
Wapiga kura walishauriwa kusimama umbali wa mita moja kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine walipokuwa wakipanga milolongo kupiga kura baada ya viwango vyao vya joto kuchukuliwa na maafisa wa afya.
Kwenye taifa jirani la Guinea waandamanaji waliwazuia wafanyikazi wa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF kuweka kituo cha ebola kusini mwa nchi hiyo.
Polisi wanasema kuwa mahema yalichomwa na wafanyikazi wakafukuzwa na megenge ya vijana.
Uchaguzi wa kuwachagua maseneta nchini Liberia
Jamii kwenye sehemu zingine za magharibi mwa afrika zilipinga jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo zikihofia kuwa huenda zikapata maambukizi kutoka kwa wafanyikazi wa kutoa huduma za afya.
Uchaguzi wafanyika nchini liberia licha ya idadi ndogo iliojitokeza kwa hofu ya kuambukizwa Ebola

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao