UCHAGUZI MKUU: Mwezi mgumu kwa Lowassa
Dar es Salaam. Kinyang’anyiro cha kuwania urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kitafikia katika hatua ngumu mwezi ujao kitakapochukua uamuzi mgumu dhidi ya baadhi ya makada wake walioonyesha nia ya kuwania urais, akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Kiongozi huyo pamoja na makada wengine sita wa CCM, walipewa kifungo cha miezi 12 kwa madai ya kuanza kampeni za urais mapema kinyume na taratibu za chama hicho iliyomalizika katikati ya mwezi uliopita na sasa wanasubiri kwa hamu, tangazo la Kamati Kuu (CC-CCM) ili wawe huru kutangaza nia ya kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho na kuendelea na shughuli nyingine za kujiandalia mazingira ya kupitishwa. Mbali ya Lowassa, wengine waliofungiwa ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba. Habari...